Pata taarifa kuu

India: Kumi wafariki, kufuatia mafuriko ya ghafla katika Milima ya Himalaya

Takriban watu kumi wamekufa na 82 hawajulikani walipo kufuatia mafuriko katika bonde katika jimbo la Sikkim, kaskazini mashariki mwa India, yanayohusishwa na kufurika kwa ziwa la barafu la Himalaya siku ya Jumatano, serikali imetangaza leo alhamisi. 

Mafuriko na maporomoko ya ardhi hutokea mara kwa mara nchini India na husababisha uharibifu mkubwa, hasa wakati wa msimu wa mvua, ambao huanza mwezi Juni hadi mwezi Septemba.
Mafuriko na maporomoko ya ardhi hutokea mara kwa mara nchini India na husababisha uharibifu mkubwa, hasa wakati wa msimu wa mvua, ambao huanza mwezi Juni hadi mwezi Septemba. REUTERS - NIHARIKA KULKARNI
Matangazo ya kibiashara

"Miili kumi imepatikana hadi sasa, na watu 82 hawajulikani walipo, wakiwemo wanajeshi," Vijay Bhushan Pathak, afisa mkuu wa serikali katika jimbo hilo, aliwaambia waandishi wa habari Jumatano jioni. Ripoti ya awali ilibaini kuwa watu watano wamefariki na makumi ya wengine hawajulikani walipo, wakiwemo wanajeshi 23, linaripoti shirika la habari la AFP.

Madaraja kumi na manne yaliharibiwa siku ya Jumatano na barabara kuu ya kitaifa inayounganisha Sikkim na maeneo mengine ya India yaliharibiwa vibaya, afisa wa kitengo cha usimamizi wa maafa katika jimbo hilo, Prabhakar Rai amesema.

Eneo hili la mbali, lenye milima la Himalaya liko karibu na mpaka wa India na Nepal. Ziwa Lhonak liko chini ya barafu karibu na Kangchenjunga, Mlima watatu mrefu zaidi duniani. Kutokana na bwawa la juu la mto, ambalo hapo awali lilikuwa limetoa maji, kiwango cha Mto Tista kilikuwa futi 15 juu kuliko kawaida, Jeshi la India limesema. 

Mabadiliko ya tabianchi

Mafuriko na maporomoko ya ardhi hutokea mara kwa mara nchini India na husababisha uharibifu mkubwa, hasa wakati wa msimu wa mvua, ambao huanza mwezi Juni hadi mwezi Septemba. Lakini kufikia mwezi wa Oktoba kipindi hicho kinakuwa kimekwisha.

Wataalamu wanasema mabadiliko ya hali ya hewa yanafanya maafa haya kuwa ya mara kwa mara na makubwa. Kuyeyuka kwa barafu pia huongeza kiwango kikubwa cha maji kwenye mito, wakati ujenzi usiofuata sheria katika maeneo yenye mafuriko pia unaweza kuzidisha uharibifu.

Barafu za Himalaya zinayeyuka kwa kasi zaidi kuliko wakati mwingine wowote kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, na kuwaweka wakazi kwenye majanga yasiyotabirika.

Barafu iliyeyuka kwa kasi ya 65% kati ya 2011 na 2020, ikilinganishwa na miaka kumi iliyopita, kulingana na ripoti iliyotolewa mwezi Juni na Kituo cha Kimataifa cha Maendeleo ya Milima ya Kimataifa.

Kulingana na njia za sasa za utoaji wa gesi chafuzi, barafu zinaweza kupoteza hadi 80% ya ujazo wake wa sasa kufikia mwisho wa karne hii, kulingana na ripoti hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.