Pata taarifa kuu
MISRI

Mauaji yatikisa nchi ya Misri wakati ikiadhimisha miaka mitatu ya mapinduzi yaliyoangusha utawala wa Hosni Mubarak

Takribani watu 29 wameuawa katika ghasia baina ya waandamanaji na polisi nchini Misri wakati Taifa hilo likiadhimisha kumbukumbu ya miaka mitatu ya mapinduzi yaliyoangusha utawala wa Rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak. Wizara ya afya imesema watu wengine 168 wamejeruhiwa kutokana na ghasia hizo.

Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Wakati ghasia hizo zikiendelea kwenye maeneo mbalimbali ya Misri, jijini Cairo katika medani ya Tahrir wafuasi wa serikali ya mpito waliendelea kushangilia miaka mitatu ya mapinduzi na kubeba mabango yenye ujumbe wa kumuunga mkono Mkuu wa Jeshi Generali Abdel Fattah al-Sisi ambaye huenda akawa Rais ajaye wa Taifa hilo.

Polisi walikabiliana nawaandamanaji wa kiislamu wanaopinga serikali ya mpito ya kijeshi huku wakimuunga mkono Rais aliyepinduliwa mwezi Julai mwaka jana Mohammed Morsi.

Hali ya usalama imezidi kuwa tete nchini humo kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara kujitokeza hususani katika vituo vya polisi, hivi karibuni kundi la Ansar Beit al-Maqdis lenye uhusiano na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda limejigamba kutekeleza mashambulizi hayo.

Wizara ya mambo ya ndani inasema waandamanji zaidi ya 1000 wanashikiliwa kwa tuhuma za kufanya vurugu.

Polisi ambao pia wanatuhumiwa kuwauawa mamia ya waandamanaji wa kiislamu toka kupinduliwa kwa Morsi wameapa kuendelea kuwadhibiti waandamanaji hao wanaotuhumiwa kukiuka sheria za nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.