Pata taarifa kuu

Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wamefariki nchini DR Congo

Nairobi – Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wanajeshi wengine wawili wa Afrika Kusini walio kwenye kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa MONUSCO, wameuwa.

Jeshi la Afrika Kusini, limethibitisha kuuawa kwa maafisa wake, ambao imesema ni kutokana na mauaji na wenyewe kwa wenyewe
Jeshi la Afrika Kusini, limethibitisha kuuawa kwa maafisa wake, ambao imesema ni kutokana na mauaji na wenyewe kwa wenyewe © RFI/Coralie Pierret
Matangazo ya kibiashara

Jeshi la Afrika Kusini, limethibitisha kuuawa kwa maafisa wake, ambao imesema ni kutokana na mauaji na wenyewe kwa wenyewe.

Tukio hilo limeelezwa kuwa, mwanajeshi mmoja alimuuwa mwenzake kwa kumpiga risasi na baadaye kujiua.

Chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika lakini,jeshi la Afrika Kusini, linasema limeanzisha uchunguzi.

Mauaji haya yametokea, wiki kadhaa, baada ya wanajeshi wengine wawili wa Afrika Kusini, walio kwenye kikosi cha nchi za Kusini mwa Afrika SADC, kuuawa baada ya kushambuliwa wakiwa kwenye kambi yao, jimboni Kivu Kaskazini.

Kumekuwa na mjadala nchini Afrika Kusini, baada ya serikali kutangaza kuwa inatuma wanajeshi 2900 kusaidia kupambana na waasi wa M 23 bila ya kuwa na vifaa vya kutosha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.