Pata taarifa kuu

Uganda: Mahakama ya Katiba yakataa rufaa dhidi ya sheria yenye utata dhidi ya ushoga

Mahakama ya Katiba nchini Uganda leo Jumatano Aprili 3 imekataa rufaa dhidi ya sheria kandamizi dhidi ya ushoga iliyopitishwa mwezi Mei 2023 katika nchi hii ya Afrika Mashariki, ambayo ilikasirisha Umoja wa Mataifa na mashirika ya haki za binadamu na kusababisha Marekani kuchukuwa vikwazo.

Rasimu hiyo inayoitwa "sheria ya kupinga ushoga 2023", inatoa adhabu kali kwa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na "kukuza" ushoga. Kosa la "ushoga uliokithiri" unaadhibiwa na hukumu ya kifo, hukumu ambayo, hata hivyo, haijatumika kwa miaka mingi nchini Uganda.
Rasimu hiyo inayoitwa "sheria ya kupinga ushoga 2023", inatoa adhabu kali kwa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na "kukuza" ushoga. Kosa la "ushoga uliokithiri" unaadhibiwa na hukumu ya kifo, hukumu ambayo, hata hivyo, haijatumika kwa miaka mingi nchini Uganda. AP
Matangazo ya kibiashara

Rasimu hiyo inayoitwa "sheria ya kupinga ushoga 2023", inatoa adhabu kali kwa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na "kukuza" ushoga. Kosa la "ushoga uliokithiri" unaadhibiwa na hukumu ya kifo, hukumu ambayo, hata hivyo, haijatumika kwa miaka mingi nchini Uganda.

Awali wakili wa upande wa walalamishi alifahamisha kwamba uamuzi huo unaweza kusisitiza kuongezeka kwa ukandamizaji dhidi ya mashoga barani Afrika, ikiwa ni pamoja na nchini Ghana ambapo wabunge walipitisha sheria kali dhidi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Mwaka 2022, serikali ya Uganda ilipiga marufuku na kusimamisha shughuli za Shirika linalowatetea mashoga kwa sababu halikuwa limesajiliwa rasmi.

Mahusiano ya watu wa jinsia moja yameharamishwa nchini Uganda tangu enzi ya ukoloni wa Uingereza na nchi hiyo kutunga mojawapo ya sheria kali zaidi duniani dhidi ya LGBT mwezi Mei, na kuharamisha ukuzaji wa ushoga nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.