Pata taarifa kuu

DRC: Raia wanaendelea kusubiri kuundwa kwa serikali mpya

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ni siku kumi baada ya kuteuliwa kwa Judith Suminwa kuwa Waziri Mkuu, mwanamke wa kwanza katika historia ya nchi hiyo kushika nafasi hiyo, bado hajakabidhiwa ofisi na mtangulizi wake wa Jean-Michel Sama Lukonde.

Waziri Mkuu huyo mpya bado hajaapishwa, huku wananchi wa DRC wakiendelea kusubiri kuundwa kwa serikali mpya.
Waziri Mkuu huyo mpya bado hajaapishwa, huku wananchi wa DRC wakiendelea kusubiri kuundwa kwa serikali mpya. © Présidence - RDC
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuteuliwa na rais Felix Tshisekedi, Waziri Mkuu huyo mpya bado hajaapishwa, huku wananchi wa DRC wakiendelea kusubiri kuundwa kwa serikali mpya.

Ripoti zinasema, mtangulizi wake Jean-Michel Sama Lukonde anaendelea na majukumu ya kusimamia shughuli za uundwaji wa serikali mpya.

Inatarajiwa kuwa, serikali mpya itakuwa na Waziri wachache kidogo kinyume na ilivyokuwa kabla ya uchaguzi wa mwezi Desemba mwaka uliopita ambapo kuliwa na Mawaziri 58.

Rais wa DRC Felix Tshisekedi, akiapa Januari 20 2024.
Rais wa DRC Felix Tshisekedi, akiapa Januari 20 2024. © Presidence_RDC

Chama cha rais Tshisekedi cha UDPS kinatarajiwa kuwa na nafasi nyingi za mawaziri na nyingine kugawanywa kati ya vyama washirika waliomuunga mkono wakati wa uchaguzi.

Ripoti zinasema, chala cha UNC chake Vital Vital Kamerhe kinatarajiwa kupata nafasi tano, huku vyama vinavyoongozwa na Modeste Bahati pamoja na Jean-Pierre Bemba,vikitarajiwa kupata nafasi kwenye serikali hiyo.

Soma piaDRC: Judith Tuluka Suminwa ateuliwa kuwa Waziri Mkuu

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.