Pata taarifa kuu

Burundi: watu 100,000 wamehama makazi yao kutokana na mvua na mafuriko

Serikali ya Burundi na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini humo wamezindua ombi la msaada wa kifedha ili kukabiliana na "athari mbaya" za mvua za msimu ambazo, zikichochewa na mfumo wa hali ya hewa ya El Niño, zimewakosesha makazi karibu watu 100,000.

Mjini Bujumbura, mji mkuu wa kiuchumi na mji mkuu wa nchi ulioko kwenye mwambao wa kaskazini wa Ziwa Tanganyika, vitongoji kadhaa vimejaa maji na kusababisha mafuriko, barabara na madaraja kuharibiwa na baadhi ya hoteli na hospitali kutelekezwa kutokana na maji kuongezeka.
Mjini Bujumbura, mji mkuu wa kiuchumi na mji mkuu wa nchi ulioko kwenye mwambao wa kaskazini wa Ziwa Tanganyika, vitongoji kadhaa vimejaa maji na kusababisha mafuriko, barabara na madaraja kuharibiwa na baadhi ya hoteli na hospitali kutelekezwa kutokana na maji kuongezeka. © YASUYOSHI CHIBA/AFP
Matangazo ya kibiashara

Afrika Mashariki imekuwa na mvua kubwa katika wiki za hivi karibuni na kusababisha vifo vya takriban watu 58 nchini Tanzania katika nusu ya kwanza ya mwezi Aprili na wengine 13 nchini Kenya.

Nchini Burundi, nchi maskini zaidi duniani kwa pato la mtu mmoja mmoja kwa mujibu wa Benki ya Dunia na mojawapo ya nchi 20 zilizo katika hatari kubwa ya kukabiliwa na mabadiliko ya hali ya hewa kulingana na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), mvua zilikuwa karibu bila kukatizwa mwezi Septemba, badala ya misimu miwili ya mvua ya kawaida (Septemba-Januari na Machi-Mei).

Kwa jumla, kati ya mwezi Septemba na Aprili 7, "watu 203,944 waliathiriwa" na mafuriko, maporomoko ya ardhi, upepo mkali na mvua ya mawe, na "idadi ya wakimbizi wa ndani iliongezeka kwa 25% hadi kufikia watu 96,000", Waziri wa Mambo ya Ndani, Martin Niteretse, na mratibu mkazi wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi, Violet Kenyana Kakyomya walisema siku ya Jumanne katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Taarifa hiyo kwa vyombo vya habari pia inaripoti "watu waliopoteza maisha", bila kutoa tathmini, "uharibifu wa mashamba ya mazao, njia za kujikimu, nyumba na miundombinu ya kijamii na kiuchumi". Wakati utabiri wa hali ya hewa unatabiri mvua itakuwa kwenye "kiwango cha juu" hadi mwezi Mei, "serikali na wahusika wa misaada ya kibinadamu wanahitaji rasilimali za kifedha ili kukabiliana na changamoto zinazoongezeka ili kuepuka kuzorota" kwa hali hiyo, wametoa wita.

Kwa jumla, watu 306,000 "wanahitaji msaada wa kibinadamu". Serikali ya Rais Evariste Ndayishimiye imekuwa ikikabiliwa na ukosoaji kwa wiki kadhaa, haswa kutoka kwa mashirika ya kiraia na upinzani, ambao wanato wito wa kutangazwa kwa "hali ya maafa ya asili" au "hali ya hatari".

Mjini Bujumbura, mji mkuu wa kiuchumi na mji mkuu wa nchi ulioko kwenye mwambao wa kaskazini wa Ziwa Tanganyika, vitongoji kadhaa vimejaa maji na kusababisha mafuriko, barabara na madaraja kuharibiwa na baadhi ya hoteli na hospitali kutelekezwa kutokana na maji kuongezeka. Maji ya ziwa la pili kwa ukubwa barani Afrika yalifikia mita 777.04 mnamo Aprili 12, cm 36 kutoka kwa rekodi ya mafuriko ya mwaka 1964, mkuu wa kikosi jamii, Jenerali Anicet Nibaruta, alionya siku ya Ijumaa, akinukuliwa na vyombo vya habari vya Burundi.

El Niño, ambayo ilianza katikati ya mwaka 2023 na inaweza kudumu hadi Mei, imekuwa na matokeo mabaya mara kwa mara katika Afrika Mashariki. Mwezi Desemba, zaidi ya watu 300 walikufa katika maafa mbalimbali yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha. Kuanzia mwezi Oktoba 1997 hadi Januari 1998, mafuriko makubwa yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 6,000 katika nchi tano za eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.