Pata taarifa kuu

DRC: Mji wa Kalemie washuhudia mafuriko yanayotokana na mvua kubwa

Mvua kubwa inayoendelea kunyesha imesababisha mafuriko na kukwamisha shughuli za kawaida, kwenye mji wa Kalemie nchini DRC, huku kiwango cha maji katika Ziwa Tanganyika, kikiongeka.

Mafuriko haya yanajiri wakati huu kiwango cha maji katika Ziwa Tanganyika, kikiongeka.
Mafuriko haya yanajiri wakati huu kiwango cha maji katika Ziwa Tanganyika, kikiongeka. RFI
Matangazo ya kibiashara

Watu zaidi ya Elfu tatu wameyakimbia makaazi yao huku miundombinu ikiharibika.

Mji wa Kalemie umegawanyika kwa sehemu mbili, Barabara ya  Lumumba ambayo ni barabara kuu inayounganisha sehemu ya mji na mtaa wa Lukuga, inafunikwa na maji kwa zaidi ya mita 100.

Ziwa Tanganyika linalotenganisha Tanzania na nchi nyingine jirani kama Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Juni 10, 2023
Ziwa Tanganyika linalotenganisha Tanzania na nchi nyingine jirani kama Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Juni 10, 2023 © Steaven Mumbi, RFI Kiswahili

Magari machache tu ndio bado yanajaribu kutumia barabara hii, wakati huu baadhi wakilazimika kuvuka kwa kutumia mtumbwi.

Mbali na kuongezeka kwa viwango vya maji katika Ziwa Tanganyika, mito inayozunguka mji wa Kalemie,nayo pia imefurika. Kwa mujibu wa mashirika ya kiraia, zaidi ya jamaa 3,500  wameathirika na janga hili. 

Soma piaDRC: Takriban watu 8 wafariki kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha Kinshasa

Idadi ya wanaothirika na mafuriko haya inaendelea kuongezeka wakati hii familia nyingi zikiyahama makazi yao. Baadhi ya miundombinu kama vile hoteli na shule zimeharibiwa .

Jules Mulya, kiongozi wa wafanyibiashara katika eneo hili , anaeleza kuwa shughuli za kiuchumi pia zinaathirika. Nyumba nyingi za biashara zimefurika maji.

Raia wa Kongo wakusanyika baada ya kifo cha wanafamilia wao kufuatia mvua kubwa iliyoharibu majengo katika kijiji cha Nyamukubi, eneo la Kalehe katika jimbo la Kivu Kusini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mei 6, 2023 .
Raia wa Kongo wakusanyika baada ya kifo cha wanafamilia wao kufuatia mvua kubwa iliyoharibu majengo katika kijiji cha Nyamukubi, eneo la Kalehe katika jimbo la Kivu Kusini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mei 6, 2023 . REUTERS - STRINGER

Kwa upande wake, waziri wa miundombinu wa jimbo hilo, John Seya, ameeleza  kuwa jimbo la Tanganyika  halina uwezo kifedha wa kukabiliana na janga hili.

Denise Maheho- Lubumbashi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.