Pata taarifa kuu

Uganda: Wafanyabiashara wagoma kulalamikia mfumo mpya wa utozwaji kodi

Nchini Uganda, wafanyabiashara jijini Kampala na miji mingine wanaendelea na mgomo baada ya kukataa wito wa serikali wa kufungua maduka yao.

Wafanyabiashara wengi wamekataa wito wa kufungua maduka yao wakitaka serikali pamoja na rais Yoweri Museveni aingilie kati kwa haraka.
Wafanyabiashara wengi wamekataa wito wa kufungua maduka yao wakitaka serikali pamoja na rais Yoweri Museveni aingilie kati kwa haraka. AP - Bebeto Matthews
Matangazo ya kibiashara

Wafanyakazi hao wanalalamikia mfumo mpya wa utozwaji kodi, wanaosema utawasababishia hasara.

Waziri wa Fedha Matia Kasaija alitoa wito kwa wafanyabiashara hao kufungua maduka yao huku Serikali ikizingatia matatizo yao ndani katika muda wa wiki mbili zijazo.

Wito huo ulijadiliwa katika mkutano wa wafanyabiashara. Thaddeus Musoke ni kiongozi wa wafanyabiashara

“Wafanyabiashara wengi wamekataa wito wa kufungua maduka yao. Kwa hiyo tunaiomba Serikali pamoja na rais aingilie kati kwa haraka.” Thaddeus Musoke ni kiongozi wa wafanyabiashara.

00:11

Thaddeus Musoke ni kiongozi wa wafanyabiashara

Serikali ilikuwa imemtuma waziri anayesimamia mji mkuu wa Kampala Kabuye Kyofatogabye kuwashawishi kuachana na mgomo huo lakini alishindwa kuapata suluhu.

“Wale wanaotaka kufanya kazi wanaweza kwenda na kufungua na tutawapa usalama. Wale ambao hawataki wanaweza kwenda nyumbani na kusubiri labda kwa mkutano na rais siku ya Ijumaa. Chaguo ni lao. ” Kabuye Kyofatogabye waziri anayesimamia mji mkuu wa Kampala.

00:15

Waziri anayesimamia mji mkuu wa Kampala Kabuye Kyofatogabye

Wafanyabiashara hao wanasema kuwa mfumo wa ushuru ni wa gharama kubwa  kuutumia. Pia wanasema wanatozwa ushuru mkubwa kwa nguo zinazoagaizwa nje ya nchi.

Mwanauchumi Africa Kiiza alikuwa na mtazamo huu kuhusu kinachoendelea kushuhudiwa kwa sasa.

“Mfumo wetu wa kodi sio sawa na biashara zinazotozwa kodi.” aliezaMwanauchumi Africa Kiiza.

00:18

Mwanauchumi Africa Kiiza

Kampala bado iko chini ya ulinzi mkali huku wafanyabiashara wakiendelea na mgomo wao. Wafanyibiashara hao wanatumai kuwa rais anayepanga kukutana nao siku ya Ijumaa ataingilia kati.

Kenneth Lukwago, Kampala-RFI Kiswahili

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.