Pata taarifa kuu

Kenya: Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali Francis Ogola alikuwa nani?

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kupitia mtandao wake wa kijamii wa X, ametuma salamu za pole kwa Wakenya kufuatia kifo cha Mkuu huyo wa Majeshi ya Kenya, salamu ambazo pia zimetumwa na Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika Mousa Faki, Jumuiya ya IGAD na ubalozi wa Marekani na Uingereza nchini Kenya.

Mkuu wa majeshi ya Kenya Jenerali Francis Omondi Ogolla (katikati) akionyesha ishara wakati ziara ya Mfalme wa Uingereza Charles III (hayuko kwenye picha) na Rais wa Kenya William Ruto (hayuko kwenye picha) katika bustani ya Uhuru jijini Nairobi mnamo Oktoba 31. 2023.
Mkuu wa majeshi ya Kenya Jenerali Francis Omondi Ogolla (katikati) akionyesha ishara wakati ziara ya Mfalme wa Uingereza Charles III (hayuko kwenye picha) na Rais wa Kenya William Ruto (hayuko kwenye picha) katika bustani ya Uhuru jijini Nairobi mnamo Oktoba 31. 2023. © Tony Karumba, AFP
Matangazo ya kibiashara

Jenerali Ogola aliteuliwa na rais William Ruto kwenye nafasi hiyo mwezi Aprili mwaka uliopita, akitokea kwenye jeshi la angaa.

Hadi kifo chake, alikuwa na umri wa miaka 61, ambapo alikuwa anaelekea kutimiza mwaka mmoja kwenye nafasi hiyo na kustaafu mwaka ujao kwa mujibu wa utaratibu wa kijeshi.

Maktaba – Mkuu wa majeshi ya Kenya Jenerali Francis Ogolla, kulia, akimpa salama mfalme Charles wa tatu wa Uingereza, rais Ruto akiwa katikati. Nov. 2, 2023.
Maktaba – Mkuu wa majeshi ya Kenya Jenerali Francis Ogolla, kulia, akimpa salama mfalme Charles wa tatu wa Uingereza, rais Ruto akiwa katikati. Nov. 2, 2023. AP - Brian Inganga

Mzaliwa wa Kaunti ya Siaya, Magharibi mwa Kenya, Jenerali Ogola alijiunga na Jeshi la Kenya tarehe 24 mwezi Aprili mwaka 1984.

Kabla ya kuwa Mkuu wa Majeshi ya ulinzi, Jenerali Ogola ambaye alisomea Sayansi ya Kijeshi kutoka chuo École Militaire de Paris nchini Ufaransa, na vyuo vingine nchini Kenya, aliwahi pia kuhudumu kama rubani na mkufunzi wa ndege za kijeshi.

Soma piaKenya: Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali Francis Ogolla amefariki katika ajali

Cheo cha Mkuu wa Majeshi ya ulinzi ya Kenya maarufu kama CDF ndicho cha juu katika ngazi ya kijeshi nchini humo na kushikiliwa na Jenerali anayeteuliwa na rais aliye madarakani.

Florence Kiwuwa- Nairobi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.