Pata taarifa kuu
NIGERIA

Jonathan: Kundi la Boko Haram ni tishio kwa usalama wa mataifa ya bara la Afrika si Nigeria pekee

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ametamka wazi wazi ya kwamba Kundi la Waislam wenye Msimamo Mkali la Boko Haram ni kitisho kikubwa cha Usalama katika mataifa mengine ya Afrika na si Taifa lake pekee. 

Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan akizungumza kwenye mkutano wa Davos
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan akizungumza kwenye mkutano wa Davos REUTERS/Pascal Lauener
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo wa Nigeria amekiri vitendo ambavyo vinafanywa na Kundi la Boko Haram vinadhihirisha waziwazi ya kwamba ni kitisho kwa Wanageria lakini pia kwa mataifa mengine ya Afrika.

Rais Jonathan amesema eneo la Magharibi mwa Afrika ndilo linaweza likakabiliwa zaidi na kitisho hicho kutoka kwa Boko Haram kutokana na kuwa na wapiganaji wanaoongoza mauaji ya kujitoa mhanga.

Jonathan ameweka wazi wamekuwa wakipata taarifa Viongozi wa Boko Haram wamekuwa wakisafiri na kukutana na Viongozi wa Juu wa Mtandao wa Al Qaeda Duniani wanaowapatia msaada wa kuendelea na harakati zao.

Boko Haram ni kundi linaloshinikiza serikali ya Nigeria iweze kutambua utawala wa sharia na kupingana kabisa na mwenendo wa sasa wanaodai umegubikwa na itikadi za Mataifa ya magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.