Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
Vipindi vyote
-
Mvutano kati ya Kigali na Bujumbura, mauaji ya watu zaidi ya 10 Mwesso DRC
Yaliyojiri wiki hii inaangazia kauli ya rais wa Rwanda Paul Kagame kwamba ataitetea nchi yake kwa gharama yoyote ile, upinzani nchini Tanzania uliandamana kupinga mabadiliko ya sheria za uchaguzi, mauaji ya watu zaidi ya kumi mjini Mwesso mashariki mwa DRC, uchaguzi visiwani Komoro hali katika ukanda wa Afrika Magharibi lakini pia uchaguzi mdogo huko Marekani,27/01/202420:09 -
Kuapishwa kwa rais Felix Tshisekedi jumamosi, Rwana na UK njia panda bado
Makala hii imeangazia kuhusu kuapishwa rais wa DRC Félix Tshisekedi baada Mahakama ya katiba kuidhinisha ushindi wake katika uchaguzi wa desemba 20, viongozi wa nchi wananchama wa IGAD walikutana jijini Kampala huku wakitoa wito wa kusitishwa mapigano Sudan, waziri mkuu wa Uingereza Richy Sunak na mpango wa kuwasafirisha waomba hifadhi huko Rwanda.20/01/202420:14 -
Mahakama ya katiba yaidhisha ushindi wa Tshisekedi, Burundi yafunga mpaka na Rwanda
Mahakama ya katiba huko DRC iliidhinisha ushindi wa rais Félix Tshisekedi,rais wa Uganda Yoweri Museveni awatahadharisha waasi wa ADF, Waziri mkuu wa Uingereza Richy Sunak akabiliwa na wakati mgumu kuhusu suala la kuwasafirisha waomba hifadhi huko Rwanda, yaliyojiri katika ukanda wa Afrika Mashariki, Afrika magharibi lakini pia uteuzi wa Gabriel Attal kuwa waziri Mkuu wa kwanza kijana nchini Ufaransa, mashambulio ya jeshi la Israeli yawaathiri raia wa kawaida mjini Gaza, na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.13/01/202420:09 -
Dunia yakaribisha mwaka mpya, mvutano kati ya rais Ruto na idara ya mahakama
Miongoni mwa habari kuu za wiki hii ni pamoja na dunia kuukaribisha mwaka mpya 2024, mvutano kati ya rais wa Kenya William Ruto na idara za mahakama, wapinzani wa DRC waendelea kuonesha kutofurahishwa na ushindi wa rais Felix Tshisekedi kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi wa desemba 20 mwaka uliopita, yaliyotangazwa na CENI, yaliyojiri katika ukanda huu wa Afrika Mashariki, Afrika magharibi lakini pia mashambulio mjini Gaza, na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.06/01/202420:15 -
DRC: Rais Felix Tshisekedi ashinda uchaguzi kwa muhula wa pili
Baadhi ya habari ambazo tumeangazia ni matokeo ya uchaguzi nchini DRC ambapo Felix Tshisekedi ameshinda uchaguzi kwa muhula wa pili kwa asilimia 73.34, katika matokeo ya uchaguzi ambayo yametangazwa na Ceni Jumapili jioni.31/12/202320:01 -
Raia DRC wasubiri matokeo ya uchaguzi, Rais Biden amsuta Netanyahu kulinda raia
Kwenye makala yaliyojiri wiki hii, tumeangazia uchaguzi kule DRC wakati huu shughuli ya kuhesabu kura ikiendelea, kikosi cha jumuiya ya Afrika Mashariki chaondoka rasmi nchini DRC, mapigano kule Sudan.24/12/202320:01 -
CENI uchaguzi utafanyika desemba 20 DRC, Uingereza kuhamishia wahamiaji Rwanda
Yaliyojiri wiki hii imeangazia hatua ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini DRC CENI kusisitiza kuwa uchaguzi utafanyika desemba 20 kama ulivyopangwa; wakati huo huo aliyekuwa mwenyekiti wa CENI Corneille Nangaa alizindua chama kipya cha AFC Alliance Fleuve Congo, wabunge wa Uingereza walipiga kura kuunga mkono mpango wa kuwahamishia wahamiaji nchini Rwanda, siasa za Senegal, na huko Niger Mahakama ya ECOWAS yaamuru kuachiwa huru kiongozi aliepinduliwa nchini Niger Muhamed Bazoum, Jeshi la Israel laendeleza mashambulio mjini Gaza, na pia matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani.16/12/202320:15 -
Rwanda na Uingereza zasaini mkataba kuhusu wahamiaji, jeshi la EAC laondoka DRC
Makala hii imeangazia hatua ya Rwanda na Uingereza kutiliana saini mkataba mpya kuhusu kuwahamisha wahamiaji kutoka Uingereza kupelekwa Rwanda, makumi ya watu wapoteza maisha katika mafuriko nchini Tanzania, kampeni za uchaguzi mkuu zashika kasi kuelekea desemba 20 huko DRC, Waasi wa M23 wazidisha Mapigano eneo la mashariki mwa DRC, hali ya siasa nchini Kenya, na mataifa mengine ya Afrika magharibi, lakini pia kongamano la Kimataifa kuhusu hali ya hewa waendelea Dubai kwenye Nchi ya Falme za kiarabu, na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani...09/12/202320:15 -
Mkutano wa COP28, EU kuondoa waangalizi wake wa Uchaguzi huko DRC na mengineyo
Makala hii imeangazia mkutano wa kilele wa kimataifa kuhusu hali ya tabia nchi COP28 huko Dubai, kuachiwa kwa baadhi ya mateka waliokuwa wameshikilwia na Hamas huko Gaza, DRC ilisema muda wa Kuwepo kwa vikosi vya Jumuia ya EAC hautaongezwa baada ya desemba 08, Umoja wa Ulaya waamua kusitisha mpango wa kuwasambaza waangalizi wake wa uchaguzi nchini DRC, siasa za Kenya, Tanzania, na mengine yaliyojiri kwenye ukanda wa Afrika Mashariki, Afrika magharibi na kwengineko duniani.02/12/202320:14 -
Rais George Weah akubali kushindwa kwenye duru ya pili ya uchaguzi
Matukio kadhaa wa kadhaa yamefanyika ulimwenguni kukiwemo George Weah kukubali kushindwa katika duru ya pili ya uchaguzi nchini Liberia kwa Joseph Boakai. Hii ina maana atakuwa miongoni mwa marais waliohudumu kwa muhula mmoja.18/11/202320:03 -
Burundi kuondoa wanajeshi wake DRC, Ufaransa na mkutano kuhusu Gaza
Makala ya Yaliyojiri wiki Hii, imeangazia hatua ya kikosi cha wanajeshi wa Burundi chini ya Jumuia ya Afrika Mashariki, EAC kujiondoa maeneo ya mashariki mwa DRC, mapigano kati ya jeshi la serikali ya DR Congo FARDC na waasi wa M23 mkowani Kivu kaskazini, hotuba ya rais wa Kenya wiki hii yazua hisia mseto, hali ya kibinadamu nchini Sudan yausikitisha Umoja wa mataifa, kongamano la Kimataifa kuhusu Gaza lafunguliwa nchini Ufaransa na mengine mengi duniani.11/11/202320:15 -
Zaiara ya mfalme wa tatu wa Uingereza, kukamatwa kwa muasi wa ADF Uganda
Makala ya wiki hii imeangazia matukio kadhaa yaliyojitokeza wiki hii kote ulimwenguni, miongoni ni pamoja na ziara ya mfalme Charles wa tatu wa Uingereza nchini Kenya, ambapo pia rais wa shirikisho la Ujerumani Frank-Walter Steinmeier kule Tanzania, hali ya kisiasa na kiusalama nchini DRC, mkutano kuhusu utalii barani Afrika ulitamatika jijini Kigali, nchini Rwanda, na matukio mengine yaliyoshuhudiwa kwenye ukanda huu na kwengineko duniani.04/11/202320:18 -
Ziara ya rais E. Macron huko Israel, mapigano mashari mwa DRC, siasa za Kenya
Makala hii imeangazia ziara ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron huko Israeli, maombi kutaka bunge liidhinishe mpango wa kutumwa kwa askari wake elfu 1 nchini Haiti, hali ya kisiasa na usalama huko DRC, nchini Sudan, lakini pia hali tete ya kiafya ya kinara wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko, na matukio kadhaa yaliyoshuhudiwa kwengineko duniani. Ungana na mwanahabari wetu Ruben Lukumbuka kupata mengi zaidi28/10/202320:10 -
Mashambulio ya Gaza huko Israeli, siasa za DRC, Kenya na Burundi na mengineyo
Makala hii imeangazia ziara ya rais wa Marekani Joe Biden huko Israeli, kuuawa kwa watalii huko Uganda mpakani na DRC, siasa za Kenya na siku ya mashujaa iliyoadhimishwa oktoba 20, hali ya kisiasa na usalama huko DRC, Burundi na nchini Sudan lakini pia ziara ya rais wa Chad nchini Ufaransa, na matukio mengine mengi ya wiki hii duniani.21/10/202320:12 -
Mashambulio ya Hamas nchini Israel, siasa za DRC na ukanda wa Afrika mashariki
Miongoni mwa mengi yaliyoangaziwa katika makala ya juma hili ni pamoja na mashambulio yaliyofanywa na kundi la Hamas huko Israeli, siasa za Kenya, Uganda na Tanzania, kulegezwa kwa hali ya dharura iliyowekwa kwenye majimbo mawili ya Kivu kaskazini na Ituri huko DRC, hali ya Sudan na kuondoka kwa awamu ya kwanza ya wanajeshi wa Ufaransa nchini Niger, na mengineyo duniani.14/10/202320:14
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Makala yanayochambua masuala na matukio mbalimbali yaliyotokea kwenye jamii kwa wiki nzima kwa kina, yanatoa fursa kwa msikilizaji kueleza hisia na mtazamo wake juu ya masuala yanayoendelea kutokea iwe ni katika uga wa uchumi na siasa duniani kote.