Nyumba ya Sanaa
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
-
Fred Halla;Kutofanikiwa kwa Wachoraji kumechangia Sanaa hii Kudorora
Mchoraji Fred Halla anasema kama kungekuwepo watu waliofanikiwa katika Sanaa hii ingekuwa rahisi wazazi kuwahamasisha watoto wao kuipenda sanaa na Uchoraji,hali ilivyo sasa Uchoraji imekua ni sanaa ya ziada licha ya vipaji kuwepo.Ungana na Steven Mumbi katika Mkala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Mchoraji Fred Halla.06/11/201819:57 -
Zawose;Muziki wa asili umeniwezesha kuwa Maarufu Afrika Mashariki
Sinaubi Zawose ni kijana wa Kitanzania anayefanya Muziki wa asili akitokea katika familia yenye historia ya Muziki wa asili ya Kigogo sasa ameazimia kuufikisha Muziki huo mbali zaidi.Zawose amezungumzia safari yake ya kimuziki katika Makala ya Nyumba ya Sanaa, Ungana na Steven Mumbi katika Makala haya ya Nyumba ya Sanaa.31/10/201820:12 -
Hussein Jumbe awataka Vijana wanaofanya Muziki wa Dansi kufuata Nyayo zao
Sanaa ya Muziki wa Dansi nchini Tanzania ilianza kabla ya nchi hiyo Kupata Uhuru 1961 ,Miaka ya 1970, 1980 ndipo waliibuka wanamuziki wengi miongoni mwao ni pamoja na Mbaraka Mwishehe, Marijani Rajabu na Hussein Jumbe nae alichipukia hapo.Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa, Akizungumza na Hussein Jumbe kuhusu safari yake ya Muziki.31/10/201820:02 -
Misambano;Wanamuziki wa sasa wanachangia Taarabu Kudorora
Sanaa ya Muziki wa taarab ilishamiri sana katika nchi za Afrika mashariki miaka ya 1990 ingawaje katika nchi ya Burundi inaelezwa kuwa Watanzania ndio waliowaibua wasanii wengi nchini humo.Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa, akizungumza na Abdul Misambano msanii wa Muziki wa Taarab akiwa ni Miongoni mwa wasanii walisaidia kuikuza sanaa hiyo katika nchi za Afrika Mashariki.30/10/201819:56 -
Nyahoga;Ubunifu wa Mavazi umenifanya niheshimike
Mbunifu wa Mavazi Agnes Nyahoga anajivunia kuwa Mbunifu baada ya kufanya kazi ya kuuza chakula bila mafanikio na kuamua kufanya kazi Hotelini,akashawishika kujifunza ubunifu .Ungana na Mtayarishaji wa Makala ya Nyumba ya Sanaa Steven Mumbi kuhusu safari yake ya Ubunifu,na namna alivyofanikiwa kuifikia ndoto yake.28/09/201820:28 -
Abdul Kingo;Uchoraji wa Vibonzo umebadili Maisha ya Watawala.
Uchoraji wa Vibonzo umekua na umuhimu katika kufikisha ujumbe kwa njia ya Mchoro unaowaelezea wahusika kwa njia ya Mafumbo.Steven Mumbi amezungumza na Mchoraji wa Vibonzo Abdul Kingo, katika Makala ya Nyumba ya Sanaa kuangazia umuhimu wa Sanaa hiyo na Faida yake kwa jamii.17/09/201818:41 -
Mbanaye Bendi ya Malawi wamepania Kuutangaza Muziki wa Asili
Walianza kikiwa ni kikundi cha vijana wanane baadae ikawa bendi kamili na kusheheni muziki wa Makabila mbalimbali kutoka nchini Malawi.Katika Makala ya Nyumba ya sanaa, Steven Mumbi anazungumza na mmoja wa wasanii wa Bendi hiyo Gilbert Simchoba kuzungumzia safari ya Benki hiyo yenye miaka minne sasa.17/09/201820:50 -
Khadija Kopa;Nakubalika zaidi nikiimba Taarab za Mipasho
Muziki wa Taarabu ulianza kushamiri Miaka ya 1990 nchini Tanzania na Miongoni mwa Waanzilishi wa Bendi ya Tanzania One Theatre TOT ni Khadija Omari Kopa.Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Khadija Omary Kopa katika sehemu ya kwanza ya makala hayo.17/09/201820:04 -
Mwigune;Muziki wa Jukwaani Unalipa,Vijana tujikite
Tulizo Bendi inaundwa na vijana wa Kitanzania waliojitoa kufanya Muziki wa majukwaani,na kubadili mtizamo wa kuwa muziki ni uhuni na sasa kuwa sehemu ya maisha kwa kujikimu.Steven Mumbi anazungumza na James Mwigune Kiongozi wa Bendi hiyo inayofanya shughuli za kimuziki nchini Tanzania08/08/201820:18 -
SIGE LUCAS;Uchoraji unaakisi Maisha ya Waafrika
Sanaa ya Uchoraji picha si tu imekuwa sehemu ya ajira kwa vijana nchini Tanzania bali imekuwa sehemu ya maisha na ndoto ya watoto kuja kuwa wachoraji wakubwa,kwa kufanya kazi wanazozipenda Maishani.Ungana na Steven Mumbi akiongea na Mchoraji na Mwalimu wa sanaa hiyo Sige Lucas katika Mkala ya Nyumba ya Sanaa08/08/201819:59 -
Mariagoreth:Ushairi una nafasi ya kuleta Mabadiliko
Ushairi ni sanaa inayokua kila kukicha na watunzi wamekua na maana mbalimbali kuhusu ushairi, Senkoro (1988) Katika kitabu chake cha Ushairi, “Nadharia na Tahakiki” anasema ni utanzu wa fasihi utumiao mpangilio wa lugha ya mkato, picha, iliyopangwa kwa njia iletayo mapigo mahususi au yaliyomo ndani yake.Wamitila, (2008) ushairi ni utungo wa sanaa ya lugha na mpangilio maalum wa mishororo, ama kisauti na kwa maneno mateule kwa kubuni mbinu za lugha zenye mnato na mbinu nyingine za kibalagha na kimtindo zinamwezesha mtunzi kuwasilisha ujumbe kwa kifupi na kwa mkokotezo mkubwa unaoelezea hisia, tukio, ama hali kwa lugha ya mvuto.Kwa ujumla ushairi ni sanaa ya lugha ya mkato yenye ughunaji inayosawiri, kueleza au kuonesha jambo, hisia au katika mpangilio mahususi wa maneno wenye urari wa vina na wizani wa sauti.Kutana na Mariagoreth Charles Msanii wa kughani Mashairi kutoka Tanzania akizungumza na Steven Mumbi katika Makala haya.19/06/201820:14 -
Natasha;Utunzi wa Filamu Umepiga hatua kubwa nchini Tanzania
Uigizaji nchini Tanzania umekuwa na Historia ndefu na Waigizaji wamepitia vipindi tofauti tofauti licha ya changamoto zilizopo lakini bado filamu za kiswahili zimeendelea kustawi.Ungana na Steven Mumbi katika Makala haya akizungumzia sanaa ya uigizaji wa Filamu za Kiswahili.11/06/201820:28 -
Natty OJ ;Muziki wa Reggae umewezesha kuleta amani kwa Vijana nchini Kenya
Msanii wa Muziki wa Reggae kutoka Mombasa nchini Kenya Natty OJ anasema Muziki wake umefanikiwa kubadili mitizamo potofu ya vijana kuhusu Siasa,Uchumi na Maisha kwa Ujumla.Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Natty OJ Katika Makala haya.04/06/201820:07 -
Nsamila; Upigaji Picha ni fursa ya ajira kwa Vijana wa Kitanzania
Hapo awali Upigaji picha ilikuwa ni jambo la kujifurahisha na kutunza kumbukumbu za matukio ya kifamilia pekee na ilikuwa nadra sana,vijana kuwa na ndoto za kuwa wapiga picha hii leo imekuwa sehemu ya ajira kwa vijana wengi.Kutana na Imani Suleiman Nsamila kijana wa kitanzania aliye jiajiri kupiga picha akizungumza na Steven Mumbi kuhusu safari yake ya upigaji picha.30/05/201820:17 -
Sanaa ya Muziki wa injili na Sheila Glory
Katika makala haya utasikia kuhusu safari ya muimbaji wa muziki wa injili Sheilah Glory kutoka Kenya , alipotoka,alipo sasa na matarajio yake ya siku za usoni. Karibu10/12/201721:56
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.