Nyumba ya Sanaa
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
-
Sanaa ya uchoraji - Bikengu Iganze
Katika makala haya Bikengu Iganze anaeleza zaidi kuhusu sanaa ya uchoraji .14/08/202120:05 -
Sanaa ua usanifu wa michoro nchini Tanzania
Sanaa ya usanifu wa michoro inayotumika katika nguo ni Sanaa nyingine inayosheheneza utamaduni wa urembo katika Kanga na Vitengem mavazi maalum kwa Wanawake barani Afrika.Warda Aboubakari ni Msichana anayetamani Sanaa hiyo kutambulika viwandani, Ungana na Steven mumbi katika Makala haya ya Nyumba ya Sanaa.24/07/202120:45 -
Muziki wa singeli nchini Tanzania
Muziki wa singeli nchini Tanzania, umekuwa maarufu sana hasa jijini Dar es salaam ? Siri ni nini ? Ungana nasi.10/07/202119:53 -
Sanaa ya utengenezaji wa vibonzo
Utengenezaji wa picha jongefu ni Sanaa nyingine inayoibuka kwa kasi nchini Tanzania, Wachoraji wanatumia vipaji vyao kusanifu Michoro inayosimulia hadithi kwa njia ya video fupi ilitengenezwa kwa kutumia katuni, Je Sanaa hiyo ikoje?Ungana na Steven Mumbi katika Makala haya ya Nyumba ya Sanaa.04/07/202120:04 -
Reggae kurejea Afrika - Jah Bone D
Msanii wa Muziki wa Reggae kutoka nchini Rwanda, Jah Bone D, baada ya kuishi Uswizi kwa miaka zaidi ya 20 sasa anataka kurejesha muziki wa Reggae katika nchi za Afrika Mashariki. Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Jah Bone D katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.03/07/202120:16 -
Sanaa ya uchoraji Tanzania - Nasma Mzee
Kutana na msichana wa mwaka wa tatu Chuo kikuu cha Dar es salaam,Nasma Mzee akichukua Shahada ya Kwanza ya Sanaa na Ubunifu aliyechagua kuwa Mchoraji ili kuwasilisha Maudhui ya Sanaa aliyosomea. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Nasma Mzee.24/06/202120:04 -
Sanaa ya utunzi wa mashairi nchini Tanzania
Kutana na Mshairi Zawadi Mengele aliyejikuta akifanya Sanaa ya Ushairi baada ya kumzawadia Mama yake shairi lililo amsha hisia ya Malezi.Ungana na mwandishi wetu Steven Mumbi katika makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na mshairi huyo akianisha namna anavyopokelewa Tanzania.12/06/202120:03 -
Sanaa ya utunzi wa vitabu vya mahusiano nchini Tanzania
Ukosefu wa elimu ya mahusiano ni miongoni mwa sababu zinazochangia ndoa nyingi kuvunjika, kutana na Ahmed Hassan mtunzi wa vitabu vya mahusiano ya kimapenzi akizungumza na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa wakizungumzia Sanaa ya Utunzi wa vitabu vya mahusiano.29/05/202120:09 -
Hali ya Sanaa ya ushairi nchini Tanzania
Ushairi ni Sanaa inayokua kwa kasi, Washairi wameongeza ubunifu wakughani Mashairi sambasamba na matumizi ya Mirindimo ya Miziki inayopigwa na chombo kama ViolinUngana na Steven Mumbi katika makala ya nyumba ya sanaa akizungumza na mshairi Elizabeth Pastory.22/05/202120:18 -
Muziki wa taarab nchini Tanzania
Taarab Asilia ni Miongoni mwa Muiziki yenye asili ya Mwambao, Maudhui yanayojikita katika kuelimisha uhusiano kati ya Mume na Mke,Nyimbo zilizosheheni Majigambo ,Je Unamfahamu Afua Suleiman Maganga mtunzi wa Wimbo Utalijua jiji ?Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza nae kuhusu safari yake ya Muziki huo aliyoianza mwaka 1982.14/05/202120:18 -
Changamoto za uandishi na utunzi wa vitabu nchini Tanzania
Sanaa ya uandishi na utunzi wa vitabu ni miongoni mwa sanaa zinazofifia hivi sasa kutokana na ukuaji wa utandawaji sambamba na wasomaji wengi kugeukia utumiaji wa mitandao ya kijamii na hivyo kuathiri biashara ya uuzaji wa vitabu.Ungana na Steven Mumbi katika makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Emmanuel Mkama Mtunzi wa vitabu Kutoka nchini Tanzania wakizungumzia sanaa hiyo sambamba na Changamoto zake.17/04/202120:02 -
Muziki kutoka Uvira nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Leo tunamwangazia mwanamuziki Classic Bufreda anatueleza safari yake ya muziki. Ni mkaazi wa Uvira, Mashariki mwa DRC03/04/202120:05 -
Sanaa ya uchoraji na urembo katika mataifa ya Afrika mashariki
Uchoraji si sanaa tu inayohusisha urembo pia ni sanaa inayotumika kutunza kumbukumbu, wachoraji wanafanya sanaa hii kama sehemu mbadala ya kujipatia kipato.Augosto Ngumba ni mchoraji mwenye shahada ya elimu ya Juu katika masuala ya Jamii,baada ya kukosa Ajira akaamua kutumia kipaji chake cha uchoraji kujijiri.Ungana na Steven Mumbi katika Makala haya ya Nyumba ya Sanaa.27/03/202120:13 -
Sanaa ya ucheshi katika jamii waambatanishwa na uimbaji nchini Tanzania
Ucheshi ni Sanaa nyingine inayokua kila kukicha nchini Tanzania. Wasanii wanatumia kila mbinu ili kunasa hadhira inayohitaji kuburudika kupitia sanaa hii.Sasa Wasanii wa uimbaji waanza kuwa wabunifu kwa kubuni sanaa ya Uimbaji kupitia Ucheshi, Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Kundi la MAHONA OLD SCHOOL CREW katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.13/03/202120:03 -
Sanaa ya uchoraji naye Thobius Minzi
Sanaa ya Uchoraji nchini Tanzania imeendelea kudhihirisha uzuri wa Utamaduni uliopo nchini Tanzania,Wachoraji wanajikita kuhifadhi Historia kupitia picha na wengine kufanya sanaa hiyo kwa kuchora picha halisia.Thobius Minzi ni Mchoraji anayechora picha kwa kutimia kalamu za risasi na baadae hutumia rangi za Cliric.Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akiangazia sanaa ya Uchoraji.06/03/202119:59
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.