Nyumba ya Sanaa
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
-
Maudhui katika sanaa ya filamu nchini Kenya
Serikali ya Kenya imeendelea kutilia mkazo suala la kukagua maudhui ya kazi za sanaa nchini humo kwa lengo la kuhakikisha kuwa, ujumbe wa filamu na muziki sio wa kupotosha. Tunaangazia hili na afisa katka bodi ya filamu nchini humo Bonventure Kioko.16/11/201920:08 -
Wamwiduka wakifanya Onesho Mtaani
Bendi ya Muziki inayofanya Sanaa ya Muziki kwa kupiga mtaa kwa Mtaa wazungumzia namna walivyofanikiwa kuifanya sanaa hiyo kutokea mkoani Mbeya Nyanda za juu kusini mwa Tanzania mpaka jijini Dar es salaam kufanya sanaa hii.Ungana na Steven Mumbi katika Makala haya akizungumza na Viongozi wa Bendi hiyo.12/11/201920:06 -
Koshuma; Sanaa ya Urembo inalipa zaidi ya Kuajiriwa
Sanaa ya Urembo ni Sanaa nyingine inayokuwa kwa kasi miongoni mwa Vijana, Wasichana wanatumia fursa ya kuwaremba si Maharusi tu hivi sasa hata watu wa kawaida wanapenda kurembwa katika sura zao ili kuonekana warembo na Watanashati katika shughuli zao za Kawaida.Makala haya yameangazia Sanaa hii, Steven Mumbi amezungumza na Hilda Koshuma, Mwalimu na Msanii anayefanya Sanaa hii31/10/201920:07 -
Ngumba; Uchoraji wa Picha Halisi unavutia Watalii
Sanaa ya Uchoraji wa picha Halisi ni Sanaa nyingine inayopendwa nchini Tanzania, kutana na Mchoraji Agasto Ngumba akizungumzia Sanaa hiyo katiak Makala haya.14/10/201920:03 -
Wadatoga na Wamasai wanajivunia Sanaa ya Uimbaji nchini Tanzania
Wadatooga (pia huitwa Wataturu au Wamang'ati) ni kabila la watu wa Kiniloti nchini Tanzania wanaoishi hasa katika mikoa ya Manyara, Mara, Arusha na Singida.Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na kikundi cha WADACA kutoka Ngorongoro kaskazini mwa Tanzania.14/10/201920:01 -
Kutana na Mchoraji wa Vibonzo 'Muhidin Msamba'
Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Mchoraji wa Vibonzo Muhidini Msamba kuhusu safari yake ya sanaa na Mapokeo ya sanaa hiyo kwa Ujumla.26/08/201920:05 -
Malkia Queens; Wasichana Wasanii wanaojivunia kuwa Wachoraji
Upatikanaji wa Vifaa,Gharama pamoja na Uelewa Duni vinachangia Sanaa ya Uchoraji kushindwa kusonga Mbele.Malkia Queens wazungumza na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.11/06/201920:07 -
Monalisa;Kazi za Sanaa za Wanawake hazijanadiwa vya kutosha
Makala ya Nyumba ya Sanaa inaangazia changamoto wanazokabiliana nazo wanawake Waigizaji kiasi cha kuwalazimisha kugeukia kazi nyingine ili kujipatia kipato.Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Wasanii mbalimbali nchini Tanzania.11/06/201920:05 -
Wawanawake waaswa kujitokeza kufanya Sanaa za Mikono
Nyumba ya Sanaa inaangazia Sanaa ya Ususi ama Ufumaji kutoka Mkoani Morogoro Nchini Tanzania.Mtangazaji wa Makala haya Steven Mumbi anazungumza na Kiongozi wa Kikundi cha Mkonge Sisal.11/06/201919:57 -
Maembe; Muziki wa asili una changamoto Nyingi
Vitali Maembe azungumzia safari yake ya Kimuziki na Maisha hasa anavyokwamishwa kufikia Malengo yake.11/06/201920:26 -
Hali ya Muziki na Wanamuziki wa Tanzania
Kutana na Imelda Munyaga Mwalimu wa Sanaa za aina mbalimbali.Katika Makala haya anazungumza na Steven Mumbi kuhusu Sanaa ya Muziki na Uigizaji.16/05/201919:57 -
'Waimbaji wa Muziki wa Injili Wabadilike'
Allain Nyangasa awataka Waimbaji wa Muziki wa Injili kubadilika kufanya Muziki wa Injili kwa ajili ya kumtumikia Mungu na si BiasharaUngana na Steven Mumbi katika Makala haya akizungumza na Msanii huyo.29/04/201920:00 -
Mloka;Ushairi wa zamani ulikuwa unakonga nyoyo za Wengi
Ushairi ni Sanaa iliyotumika kukuza Lugha ya Kiswahili katika Nchi za Afrika Mashariki,ikiwemo Tanzania hasa wakati wa kupigania uhuru na hata baada ya Uhuru katika kuhamasisha watu kufanya Maendeleo.Steven Mumbi amezungumza na Mshairi wa siku nyingi nchini Tanzania,Charles Mloka, Ungana nae katika Makala haya ya Nyumba ya Sanaa.09/04/201919:59 -
S.Kide;Muziki wa Singeli Utafika mbali kama wawekezaji watajitokeza
Muziki wa Singeli ni Miongoni mwa Muziki unaochipukia nchini Tanzania,vijana wanajaribu kuifikia hadhira kwa kutumia maudhui ya Asili.Katika Makala haya ya Nyumba ya Sanaa,Ungana na Steven Mumbi akizungumzia Muziki huo akiwa na S.Kide pamoja na Kiongozi wa Wakupeti Band.09/04/201920:01 -
Maida;Sanaa ya Ubunifu wa Mavazi imeniwezesha kuwa Mbunifu wa Majengo
Maida waziri Mwanamke aliyeamua kufanya kazi ya Sanaa na hatimaye kufanikiwa kuwa Mbunifu wa Majengo.Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Maidfa Waziri kuhusu safari yake katika Sanaa ya Ubunifu26/03/201919:59
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.