Nyumba ya Sanaa
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
-
Usambazaji wa Filamu wawa kikwazo cha Sanaa ya Uigizaji Kuendelea Tanzania
Filamu za Kiswahili ni Miongoni mwa Filamu zinazopendwa sana katika nchi za Afrika Mashariki si kutokana na kuwa zinatumia lugha adhimu ya Kiswahili tu bali pia ni kutokana na Maudhui na upekee zilionao.Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akiangazia Sanaa hii na changamoto zinazowakabili Waigizaji nchini Tanzania19/03/201920:00 -
Cocodo; Vijana tujitume zaidi kwenye Muziki
Hii ni Sehemu ya Pili ya Makala haya tukiangazia Muziki na Cocodo African Music Band wakifanya sanaa ya Muziki kutoka nchini TanzaniaUngana na Steven Mumbi akizungumza na wasanii Remi na Nelius wakizungumzia safari yao ya kimuziki kwa zaidi ya miaka nane sasa11/03/201920:03 -
Cocodo; Vijana Hawajawekeza kufanya Muziki wa Asili kikamilifu
Katika Makala haya Tunaangazia Muziki na Cocodo African Music Band wakifanya sanaa ya Muziki kutoka nchini TanzaniaUngana na Steven Mumbi akizungumza na Lemi na Nelius wakizungumzia Safari yao ya kimuziki katika Sehemu hii ya kwanza.11/03/201920:02 -
Mubanga; Watunzi wa Vitabu Wafuate hatua za Utunzi
Teknolojia ina athari gani katika Utunzi wa Vitabu?Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Clement Mubanga Mtunzi wa vitabu katika Makala ya Nyumba ya sanaa.26/02/201919:59 -
Kimbokota; Sanaa ya Ubunifu haijawekezwa ipasavyo Mashuleni
Sanaa ya Ubinufu ndio sanaa mama katika Uchoraji,Uchongaji na hata katika matumizi ya vyuma chakavu katika kuunda Vifaa mbalimbali.Katika Makala ya Nyumba ya Sanaa Ungana na Steven Mumbi akizungumzuza na Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es salaam UDSM, Safina Kimbokota wakizungumza Sanaa hiyo na Mapokeo ya wanafunzi kusoma Sanaa katika elimu ya juu.18/02/201919:55 -
Sisi Tambala Band wataka Vijana kujikita katika Muziki wa Asili
Sisi Tambala Bendi ni Bendi ya Muziki wa Asili kutoka Tanzania, iliundwa mwaka 1997, tayari imefanya maonesho ya jukwaani katika Nchi Mbalimbali Duniani ikiwa ni pamoja na nchi za Ulaya, Asia na Afrika.Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Kiongozi wa Bendi hiyo Nanjuja Nanjuja pamoja na wasanii wanaounda bendi hiyo katika Makala ya Nyumba ya Sanaa wakizungumzia Mfanikio yao kimuziki.13/02/201920:30 -
Siku ya Upigaji Picha Duniani yaadhimishwa Tanzania
Kila mwaka Dunia huadhimisha siku ya upigaji picha za Habari, Picha zinazoelezea hali wanazokabiliana nazo wananchi katika mataifa Mbalimbali, kutoka barani Afrika ni asilimia 2 tu ya picha hizo huonekana Duniani.Katika Makala ya Nyumba ya Sanaa Steven Mumbi anaangazia umuhimu wa Upigaji Picha za Habari.06/02/201920:00 -
Belamy;Natarajia kushirikiana na Diamond katika Nyimbo zangu siku zijazo
Sanaa ya Muziki inaendelea kukua kila kukicha nchini DRC, Katika Mji wa Goma sanaa hii inasonga mbele licha ya changamoto zilizopo, anatarajia kushirikiana na wasanii wa nchi za Kenya na Tanzania katika nyimbo zake.Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Belamy Paluku katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.06/02/201920:01 -
Muziki wa Reggae utafika mbali kama Wasanii wataamka
Sixmond Mdeka Maarufu Ras Six alianza na kibao Sina Pamba kilifanya vizuri mwanzoni mwa miaka ya 2000 sasa amedhamiria kuufanya muziki wa Regae katika sura ya kisasa kuwafikia vijana zaidi kupitia Bendi yake.Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Ras Six.06/02/201919:54 -
Mussa Ngarango Jr: Wachoraji wa Vibonzo wanatamani kuishi maisha bora zaidi ya Waliyonayo
Uchoraji wa Vibonzo ni sanaa inayoshamiri kila kukicha,wachoraji wanalalama vitisho vinajitokeza katika vibonzo vinavyohusu siasa.Mussa Ngarango Jr ni Mchorajio wa Vibonzo anazungumzia sanaa hiyo katika Mkala ya Nyumba ya Sanaa akiwa na Steven Mumbi.21/01/201919:59 -
Vijana Wajitoa kufanya Saana ya Muziki Sanifu
Sanaa ya Muziki Sanifu ni uimbaji unafanyika pasipoo kutumia vyombo vya muziki wa ala, Mpangilio wa sauti kwa waimbaji ndio unasheheneza uzuri na upekee wa Sanaa hii.Kutana na Viujana wa kanisa la Anglikana Vingunguti jijini Dar es salaam,walipozungumza na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa wakielezea sanaa hiyo.21/01/201919:55 -
Waigizaji DRC walalamikia kutonufaika na Kazi zao
Waigizaji nchini DRC wanatamani Sanaa yao kufika Mbali,Miongoni mwa vikwazo wanavyokabiliana navyo ni pamoja na Uchanga wa teknolojia ikiwa ni pamoja na vifaa duni, Elimu ya Uigizaji ni suala lingine linalowarudisha nyuma.Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Kapangala Mukunda Edo Muigizaji, Mtayarishaji wa Filamu nchini DRC kutoka Goma katika Mkala ya Nyumba ya Sanaa.21/01/201920:03 -
Ras Innocent Nganyagwa; Narudi Upya Kimuziki
Muziki wa Reggae Afrika ulianza kushamiri baada ya Uhuru wa Zimbabwe Mwaka 1980, Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizokuwa za mwanzo kupata mapokeo ya Muziki huo.Ras Innocent Nganyagwa ni Miongoni mwa wanamuziki waliochipuka katika kizazi cha tatu cha Muziki huo kutoka Tanzania, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumzia na Ras Inno kuhusu ujio Wake Mpya katika Sanaa hiyo.12/12/201820:04 -
Mgogosi;Nakomaa na Muziki unitoe kimaisha
Mwanamuziki Chipukizi Ernest Mgogosi amejikuta akiingia kwenye Muziki baada ya kukutana vikwazo wakati akisoma Chuo cha Sanaa ili kuwa Muigizaji Mkubwa.Mtayarishaji wa Makala ya Nyumba ya Sanaa Steven Mumbi amezungumza na Frank Ernest Mgogosi kuangazia safari yake ya kimuziki na namna anavyojipanga kuiteka Hadhira.06/11/201820:17 -
Fred Halla;Kutofanikiwa kwa Wachoraji kumechangia Sanaa hii Kudorora
Mchoraji Fred Halla anasema kama kungekuwepo watu waliofanikiwa katika Sanaa hii ingekuwa rahisi wazazi kuwahamasisha watoto wao kuipenda sanaa na Uchoraji,hali ilivyo sasa Uchoraji imekua ni sanaa ya ziada licha ya vipaji kuwepo.Ungana na Steven Mumbi katika Mkala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Mchoraji Fred Halla.06/11/201819:57
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.