Nyumba ya Sanaa
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
-
Sagna: Msani wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania
Sagna ni miongoni mwa wasanii wachache kutoka kanda ya ziwa wanaofanya sanaa ya Muziki wa kizazi kipya, anapambana kufanikiwa licha ya changamoto. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.22/04/202320:02 -
Nyimbo za taarabu zinavyokubalika na mashabiki wa muziki huo: Rahma Machupa
Naomba Stara ni miongoni mwa nyimbo za taarabu zinazokubalika na mashabiki wa muziki huo, katika eneo la Afrika mashariki na kati ambapo Rahma Machupa ndie muimbaji wa kibao hicho. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza nae huku ukipata vionjo vya muziki wake mtamu.08/04/202320:07 -
Vionjo vya muziki wa Bongo Fleva
Makala ya Nyumba ya Sanaa ya juma hili inakuletea muziki wa Bongo Fleva ambao sasa unachagizwa na vionjo vipya, wasanii wachanga wanajiimarisha kwa kubobea na kutoa ladha inayokonga nyoyo za wapenzi waliokata tamaa, kutana na Zack Muziki akizungumza na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.01/04/202320:04 -
SANAA NA ELIZABERT PASTORY KUHUSU USHAIRI
Kwenye makala ya wiki hii Steven Mumbi amezungumza naye Elizabert Pastory kuhusu Ushairi.13/03/202320:01 -
20:08
-
Sanaa ya Muziki na Zach Music
Kwenye Makala ya wiki hii Steven Mumbi anazungumza naye Zach Music kuhusu masuala ya sanaa ya Muziki.13/03/202320:04 -
Sanaa ya Muziki wa kizazi kipya
Kwenye Makala ya wiki hii ya nyumba ya sanaa, Mwandishi wetu Steven Mumbi anazungumzia kuhusu sanaa ya Muziki wa kizazi kipya.13/03/202320:11 -
Namna ya kuhifadhi ala na miziki ya kale nchini Kenya
Ala za muziki zilizokuwa zinatumiwa zamani katika mataifa mengi ya Afrika, zimeanza kusahaulika. Huko nchini Kenya, serikali kupitia makavazi ya Bomas of Kenya, inahifadhi ala, muziki ,na tamaduni za kale/zamani kwa lengo la kudumisha , kuhifadhi na kufundisha utamaduni wa nchi hiyo. Mengi zaidi ni katika Makala haya, yanayomshirikisha Mwandishi wetu Steven Mumbi na Victor Abuso.04/06/202220:06 -
Muziki wa Abdulrazack Habibu kutoka nchini Tanzania
Wiki hii mwandishi wetu Steven Mumbi anatoa nafasi kwa mwanamuziki Abdulrazack Habibu mwanamuziki kutoka nchini Tanzania.19/03/202220:04 -
Maendeleo ya sanaa ya muziki wa injili nchini Tanzania
Katika makala hii mwandishi wetu wa Daresalaam nchini Tanzania Steven Mumbi amejaribu kumdodosa mwanamuziki wa nyimbo za Injili maarufu sana nchini Tanzania Goodluck Gozbert kujieleza kuhusu juhudi za kukuza sanaa ya kuimba nyimbo za Injili, na mchango wao kama wanamuziki katika kufanikisha kuboreshwa maisha ya kikristo na kijamii kama ambavyo wanafanya viongozi wa kidini19/02/202220:05 -
Sanaa ya muziki ushairi inavyotia fora nchini Tanzania
Sanaa ya muziki ushairi ni sanaa nyingine iliyosheheni tenzi za mafu,bo.zilizobeba ujumbe sambamba na matumizi ya nahau na Methali za lugha adhimu ya kiswahili.Kutana na Mrisho Mpoto almaarufu Mjomba katika makala ya Nyumba ya Sanaa na mwandishi wetu Steven Mumbi.15/01/202220:09 -
Muziki wa taarabu unavyotia fora nchini Tanzania hadi sasa
Makala hii ni mwendelezo wa mazungumzo ya mwandishi wetu Steven Mumbi na msanii wa muziki wa taarabu nchini Tanzania Afue Maganga ambaye ameonesha kuwa Taarab ni nyimbo zilizosheheni majigambo hasa kwa wanawake wakitambiana, wake wenza kuibana wanaume na mambo mengineUngana na mwandishi wetu Steven Mumbi kupata mengi zaidi.18/12/202119:53 -
Sanaa ya muziki wa taarab katika maendeleo ya jamii ya kisasa
Nyumba ya sanaa inakuletea vionjo vya muziki wa taarab tangu zama za kale, chimbuko lake lakini pia mchango wa sanaa ya muziki huu katika maendeleo ya jamii wakati huu ulimwengu ukiinukia teknolojia mpya, na mabadiliko ya mambo mengi.Ungana na mwandishi wetu Steaven Mumbi na mgeni wake msanii wa Taarabu kule Tanzania Afua Suleimann Maganga11/12/202119:55 -
Tanzania - Sanaa ya muziki naye Nguza Viking
Nguza Viking ni Miongoni mwa Wasanii wa Muziki wa zamani waliopitia Misukosuko hasa baada ya kufanya sanaa nchini Tanzania kwa Mafanikio .Ungana na Stephen Mumbi katika Makala haya akizungumza na Nguza Viking.07/12/202120:06 -
DRC - sana ya muziki Dakta Cow B London
Stephen Mumbi, anazungmza na mwanamziki Dakta Cow B London, kutoka Jumhuri ya Kidemokrasia ya Congo.06/12/202120:02
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.