Nyumba ya Sanaa
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
-
TMK Maandishi 3 wamedhamiria kubadili mtizamo kuhusu Muziki wa kizazi kipya
Mwandishi wa Dar es Salaam Steven Mumbi amezungumza naye Moses Francis maarufu Doro ambaye ni miongoni mwa wale waliounda TMK12/08/202320:06 -
Muziki wa Reggae nchini Tanzania
Muziki wa Reggae ni Sanaa iliyofifia nchini Tanzania, miongoni mwa sababu zinazotajwa ni pamoja na kudorora kwa matamasha ya muziki huo, Steven Mumbi anazungumza na Paul Mihambo mwanamuziki wa Reggae nchini humo.05/08/202320:01 -
20:05
-
Sanaa ya Muziki wa Hip Hop nchini Tanzania
Yessaya Cleophace Maarufu PMawenge Msanii wa Hip Hop anasema Muziki huo hauthaminiwi kama Muziki wa Kizazi kipya, sasa anakuja kitofauti kuleta ladha Mpya22/07/202320:02 -
Vijana wanaofanya sanaa ya muziki wa bongo fleva kutoka Dar es salaam
Abby love na Addo Six, vijana wanaofanya Sanaa ya Muziki wa Bongo Fleva kutoka Dar es salaam wakizungumza na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.15/07/202320:08 -
Kasi ya sanaa ya muziki wa Injili mashariki mwa DRC kufuatia mapigano yasiyokoma
Faraja Habakuki Group ni kundi la muziki wa Injili kutoka mkowa wa Kivu Kusini eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambako vijana wadogo wameanza kujitokeza na kufanya sanaa ya muziki wa Injili, kuepukana na umasikini lakini pia hofu ya mapigano ya mara kwa mara katika eneo hilo. Ungana na Steven Mumbi akizungumza na Kundi hilo.08/07/202319:57 -
Lwiza Mbutu msani aliyedumu na bendi ya African Stars maarufu 'twanga pepeta'
Lwiza Mbutu ni Muimbaji Pekee wa Muziki wa Dansi nchini Tanzania aliyedumu na Bendi ya African Stars maarufu 'twanga pepeta' Pekee tangu kuasisiwa kwa Bendi hiyo mwaka 1998, nini siri, Steven Mumbi amezungumza na Lwiza Mbutu Makala ya Nyumba ya Sanaa .01/07/202320:18 -
Maendeleo chanya ya muziki wa Hip Hop nchini Tanzania
Muziki wa Hip Hop kwa wanawake si jambo zoeleka katika sanaa ya muziki nchini Tanzania, kutana na msanii TK NENDEZE akizungumza na mwandishi wetu Steven Mumbi katika makala ya Nyumba ya Sanaa wiki hii.24/06/202320:03 -
Msanii chipukizi Hussein Rashid azungumzia safari yake nchini Tanzania
Mkoa wa Kigoma ,magharibi mwa Tanzania mwambao mwa ziwa Tanganyika ni miongoni mwa mikoa iliyotoa wasanii wakubwa nchini akiwemo Ali Kiba, sasa vijana Chipukizi wanaibuka kufanya sanaa hiyo. Kutana na Hussein Rashid Msanii chipukizi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.17/06/202320:04 -
Maendeleo ya sanaa ya muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania sehemu ya pili
Steve RNB ni msanii wa muziki wa kizazi kipyamakitamba na kibao Jambo Jambo kipi kilisukuma kufanya sanaa hii ya Muziki, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na msanii huyo.10/06/202320:05 -
Vanillah musics katika mabadiliko ya muziki wa kizazi kipya Tanzania
Pokea Vanillah Music ni miongoni mwa watunzi wa nyimbo na sasa kageukia uimbaji wa muziki wa kizazi kipya, kibao " Unanisitiri " ni miongoni mwa vibao pendwa. Kukipata kibao hiki kwa undani zaidi, ungana na mwandishi wetu Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na Vanillah.03/06/202320:21 -
Muziki wa kizazi kipya unavyotia fora nchini Tanzania
Makala ya Nyumba ya Sanaa ya juma hili, inamwangazia msanii Steven Charles almaarufu Samertz ni mtayarishaji wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania, sasa amegeukia uimbaji wa muziki huo, Je nini kimetokea kiasi cha kuanza kuimba? ungana na Steven Mumbi akizungumza na Msanii huyo katika Makala ya Nyumba ya Sanaa.27/05/202320:04 -
Maendeleo ya muziki wa Hip Hop mjini Mombasa pwani ya Kenya na Afrika Mashariki
Makala hii imejikita katika Mji wa Mombasa pwani ya Kenya kuangazia maendeleo ya muziki wa HipHop na msanii Fikra Teule ambaye katika siku za hivi karibuni aliitoa video yake mpya na sauti inayofahamika kwa jina la SEMA YOTE akiwa amemshirikisha msanii mpya katika tasnia ya muziki anayefahamika kwa jina la Victoria Gichora, ambapo uzinduzi rasmi wa video yake ulifanyika katika kituo cha utamaduni wa Ufaransa Alliance Francaise ya Mombasa na aliwashirikisha wasanii wenzake wa Hip Hop Ohms Law Montana, Azma Mponda na Mwimbaji Babs kutoka Tanzania.Fikra Teule alizitembelea studio zetu maridadi hapa RFI Kiswahili na kuhojiwa na mwandishi wetu mwandamizi Reuben Lukumbuka..20/05/202320:01 -
Nyimbo za Injili zakumbwa na mabadiliko ya kiteknolojia Afrika mashariki
Mabadiliko ya Sanaa ya uimbaji yamewafikia waimbaji wa nyimbo za Injili, sasa wanafanya Sanaa hiyo kwa kuendana na hali ya mabadiliko ya kiteknolojia kwenye sanaa ya muziki wa kisasa. Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akizungumza na muimbaji wa nyimbo za Injili Goodluck Gozbert.13/05/202320:03 -
Sanaa ya uchoraji visiwani Zanzibar
Uchoraji ni Sanaa ya Urithi, kutoka Mji Mkongwe visiwani Zanzibar urithi wa sanaa hiyo umetamalaki, Ungana na Steven Mumbi katika Makala ya Nyumba ya Sanaa akiangazia sanaa hiyo.06/05/202320:06
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.