Pata taarifa kuu
ISRAELI-PALESTINE-Usalama

Palestina : mabomu yarindima Gaza

Juhudi za kimataifa zinaendelea ili kushawishi Israeli na Hamas kusitisha mapigano. Hata hivo idadi ya vifo inaendelea kuongezeka kufuatia mashambulizi ya jeshi la Isareli katika ukanda wa Gaza.

AFP PHOTO/MENAHEM KAHANA
Matangazo ya kibiashara

Takribani watu 20 wameuawa jumanne wiki hii, ambayo ni siku ya 15 tangu Isareli ianzishe mashambulizi yake katika ukanda wa Gaza, na kupelekea idadi ya wapalestina 593 ambao wameuawa tangu jeshi la Israeli lianze mashambulizi hayo.

Kwa mujibu wa idara ya huduma za dharura, wanawakae tisa ni miongoni mwa watu waliouawa katika mashambulizi ya leo jumanne katika ukanda wa Gaza.

Mwanamke mjamzito na msichana mdogo mwenye umri wa miaka 4 wameuawa katika mashambulizi yaliyoendeshwa katika mji wa Beit Hanoun (kaskazini) karinu na mpaka na Israeli, na wanawake wengine wawili ambao mmoja alikua na umri wa miaka 50 na mwengine 70.

Kusini mwa ukunda wa Gaza, mashambulizi ya Israeli yamemuua mwanamke mmoja katika mji wa Rafah, huku wanaume wawili wakiuawa katika mashambulizi yaliyoendeshwa katika mji wa Qarara.

Awali watu watano wamepoteza maisha na zaidi ya 70 kujeruhiwa baada ya jeshi la Israel kushambulia hospitali moja katika uanda wa Gaza.

Jeshi la Israel limesema lilikuwa linalenga ngome ya kundi la Hamas ambaye walikuwa wanatumia kuhifadhi silaha zao ndani ya hispitali hiyo.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ambaye yupo nchini Misri kujaribu kusaidia kupatikana kwa suluhu kati ya Israel na Hamas amezema serikali yake itatuma Dola Milioni 47 kuwasaidia wakaazi wa Gaza walioathiriwa

Hapo jana jumatatu, wapalestina 55 wakiwemo watoto 16 wameuawa katika mashambulizi ya jeshi la Israel. Wapalestina 11, wakiwemo watoto 5 wameuawa jana jumatatu jioni.

Watoto wanaendelea kulengwa katika mashambulizi yanayoendeshwa na jeshi la Israeli.
Watoto wanaendelea kulengwa katika mashambulizi yanayoendeshwa na jeshi la Israeli. AFP/Saïd Khatib

Familia moja yenye watu 9 wakiwemo watoto 7 waliuawa jana jumatatu katika mashambulizi yaliyoendeshwa katika mji wa Rafah, huku familia nyingine yenye watu 8, wakiwemo wato 4 waliuawa siku ya jana jumatatu katika mji wa Gaza, msemaji wa idara ya huduma za dharura amethibitisha.

Kwa jumla miili 68 iliondolewa jana jumatatu chini ya vifusi nchini Palestina.
Upande wa Israeli, wanajeshi 25 na waisraeli 2 wameuawa tangu jeshi la israeli lilipoanza mashambulizi katika ukanda wa Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.