Pata taarifa kuu
IRAN-NYUKLIA-USALAMA-DIPLOMASIA

Makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran

Makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran yaliyopitishwa katika mji wa Vienna, Austria, na nchi zenye nguvu pamoja na Iran Jumanne Julai 14 yamehitimisha miaka ya mvutano kati ya Jamhuri ya Kiislamu na jumuiya ya kimataifa.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Muhammad Javad Zarif (kulia) na kamishana wa sera za mambo ya nje wa Ulaya, Federica Mogherini, walifanya mkutano na wanahabari kurasimisha mkataba huo. Vienna, Julai 14 mwaka 2015.
Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Muhammad Javad Zarif (kulia) na kamishana wa sera za mambo ya nje wa Ulaya, Federica Mogherini, walifanya mkutano na wanahabari kurasimisha mkataba huo. Vienna, Julai 14 mwaka 2015. AFP PHOTO / JOE KLAMAR
Matangazo ya kibiashara

Tehran na nchi "5 + 1" zenye nguvu zimefunga ukurasa wa diplomasia ya kimataifa, lakini ukurasa mwengine umefunguliwa. Tarehe za mikutano zimepangwa na kazi imeanza sasa.

Makubaliano kuhusu mpango wa nyuklia ya Iran iliyopitishwa siku ya Jumanne yanasimamia kwenye nguzo tatu: kuweka kikomo katika mpango wa uzalishaji wa nyuklia angalau kwa kipindi cha miaka kumi; kuondoa vikwazo vya kimataifa dhidi ya Iran; kudhibiti ukaguzi.

Mpango wa nyuklia wa Iran hautafutwa, lakini utawekewa kikomo. chini ya hali yoyote Iran haitapata au kuendeleza silaha za nyuklia. Uamzi huu uliopendekezwa na Ufaransa unapatikana sasa katika utangulizi wa nakala ya makubaliano. Na kuhakikisha kuwa uamzo huo unaheshimishwa, mpango wa nyuklia wa Iran utasimamiwa na kufuatiliwa kwa karibu. Wakaguzi wa shirika la kimataifa la nishati ya Nyuklia (IAEA), watakua wakikagua maeneo ya Iran, hata ya kijeshi.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI katika mji wa Vienna, Sami Boukhelifa, makubaliano haya pia hutoa mchakato wa kubadilishwa, "snap back". Katika suala la ukiukwaji au uvunjwaji wa makubaliano, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itachukuliwa vikwazo vipya. Inatosha tu moja ya nchi "5 + 1" zenye nguvu kuchochea mchakato huo.

Obama yuko tayari kupinga kwa kura ya turufu

Makubaliano haya yanapaswa sasa kuwa chini ya azimio la Umoja wa Mataifa. Jumanne asubuhi wiki hii, mawaziri wa mambo ya nje wa nchi zenye nguvu wametia saini kwenye rasimu ya azimio ambayo ilitumwa mara moja kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Kuanzia wiki ijayo, Baraza la Usalama litaiidhinisha". Kwa maneno mengine, kuipitisha.

Wakati huo huo utawala wa Obama utawasilisha nakala hii ya makubaliano kwenye ofisi ya Bunge la Congress. Wabunge wa Marekani wana miezi miwili ya kuijadili na kuipitisha. Barack Obama tayari ameonya. Amesema atatumia kura yake ya turufu ili iweze kupitishwa. " Nitapinga kwa kutumia kura yangu ya turufu kwa sheria yoyote ambayo itakuja kuzuia utekelezaji wa mkataba huu ", amesema rais Barack Obama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.