Pata taarifa kuu
YEMEN-MASHAMBULIZI-USALAMA

Yemen: muungano wazidisha mashambulizi yake ya anga

Ndege za muungano wa Kiarabu zimezidisha mwishoni mwa wiki hii mashambulizi yake ya anga dhidi ya waasi nchini Yemen, hasa katika mji mkuu Sanaa, katika kulipiza kisasi kwa mashambulizi yaliyowaua askari wake 60.

Moshi ukifumba kutoka majengo katika mji wa Sanaa, ambao umeshuhudia mashambulizi ya anga yakiendehwa na Saudi Arabia, Septemba 6, 2015.
Moshi ukifumba kutoka majengo katika mji wa Sanaa, ambao umeshuhudia mashambulizi ya anga yakiendehwa na Saudi Arabia, Septemba 6, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Baada ya mashambulizi makali Jumamosi, ndege za muungano unaoongozwa na Saudi Arabia zimeendelea na mashambulizi ya anga Jumapili hii zikilenga ngome nyingi za waasi wa Kishia wa Huthi katika mji mkuu wa Yemen, Sanaa.

Raia wa mji mkuu wa Sanaa wameamshwa mapema asubuhi kwa milio na milipuko ya mabomu, na wakati huo walianza kukimbia vitongoji, mashahidi wamesema.

" Shambulizi la kwanza liliiitikisa nyumba yangu ", mkaazi mmoja, Sadeq al-Juhayfi, ameeleza.

Muungano wa Kiarabu unaundwa na nchi nyingi za Ghuba. Uliingilia kati tangu miezi kadhaa iliyopita kwa kumsaidi Rais wa Yemen Abd Rabbo Mansour Hadi, ambaye aliikimbia nchi yake mwezi Februari baada ya waasi wa Huthi kudhibiti sehemu kubwa ya nchi kwa msaada wa vikosi vinavyomuunga mkono Rais wa zamani Ali Abdullah Saleh.

" Tuko tayari kudhibiti hali ya mambo nchini Yemen ", amesema, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Umoja wa Falme za Kiarabu, Sheikh Mohammed bin Zayed Al-Hahyane, Mwanamfalme mrithi wa Abu Dhabi na mkuu wa majeshi , akimaanisha waasi.

Ndege za muungano zimelenga ikiwa ni pamoja na makao makuu ya vikosi vya usalama katika mji wa Hadda, kusini mwa Sanaa, pamoja na ngome za waasi wa Huthi katika maeneo ya kaskazini mwa mji.

Ghala za silaha za Jebel Neqm, zinazodhibitiwa na vikosi vinavyoshirikiana na waasi, mashariki ya Sanaa, na ikulu ya rais pamoja na ngome zilio karibu na balozi za Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu pia zimeshambuliwa, mashahidi wamesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.