Pata taarifa kuu
PALESTINA-ISRAEL-MAUAJI-USALAMA

Raia mmoja wa Palestina awarushia risasi wanajeshi wa Israel

Mpalestina mmoja amewashambulia kwa risasi wanajeshi wa Israel Jumanne hii kabla ya kuuawa kwa kupigwa risasi katika Ukingo wa Magharibi, jeshi la Israel limebaini.

Makabiliano kati ya waandamanaji wa Palestina na jeshi la Israel, Novemba 16, 2015 katika mji wa al-Bireh karibu na Ramallah.
Makabiliano kati ya waandamanaji wa Palestina na jeshi la Israel, Novemba 16, 2015 katika mji wa al-Bireh karibu na Ramallah. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Hakuna mwanajeshi ambaye aliuawa wala kujeruhiwa katika shambulio hilo lililotokea karibu na kijiji cha Palestina cha Turmus Ayya, kaskazini mwa Ramallah, jeshi la Israel limeongeza katika taarifa yake, huku ikibaini kwamba limewakamata raia wawili wa Palestina katika eneo la shambulio.

"Risasi zimepigwa dhidi ya wanajeshi ambao wamekua wakipiga doria", wakati huo huo vikosi vilijibu kwa kurusha risasi," jeshi limebaini. Mshambuliaji mmoja "ameuawa na washukiwa wawili wamekamatwa papo hapo."

Maafisa wa kijeshi wamethibitisha kifo cha mshambuliaji. Haijaeleweka kamacWapalestina hao wawili waliokamatwa walishiriki katika shambulio hilo.

Viongozi wa usalama wa Palestina pia wamethibitisha kifo cha Mpalestina huyo, wakisema kuwa alikua ndani ya gari alipokuwa akirusha risasi.

Shambulizi hili ni moja ya mashambulizi ya hivi karibuni katika mlolongo wa machafuko yalioibuka mapema mwezi Oktoba kati ya Waisrael na Wapalestina.

Jumatatu wiki hii, Wapalestina wawili waliuawa katika makabiliano na jeshi la Israel ambalo liliingilia kati katika kambi ya wakimbizi ya Qalandiya katika Ukingo wa Magharibi kwa kubomoa nyumba ya mtu aliyehusika na shambulio dhidi ya Waisrael.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.