Pata taarifa kuu

Mashirika matatu ya kimataifa yasitisha shughuli zao nchini Afghanistan

Mashirika matatu ya kimataifa nchini Afghanistan yamesitisha shughuli zao. Shirika la Save the Children, CARE na shirika linalohudumia Wakimbizi la Norway yanadai kwamba wanaume na wanawake wanaweza kutekeleza misheni yao ya usaidizi kwa njia sawa. Jumamosi hii, Desemba 24, Taliban walipiga marufuku vyama na mashirika yasiyo ya kiserikali, kitaifa na kimataifa kuwaajiri wanawake, kwa misingi ya kutofuata uvaaji wa hijabu ya Kiislamu.

Wanawake wa Afghanistan wanasubiri kupokea pesa katika kituo cha usambazaji kilichoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani (WFP) huko Kabul mnamo Novemba 20, 2021.
Wanawake wa Afghanistan wanasubiri kupokea pesa katika kituo cha usambazaji kilichoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani (WFP) huko Kabul mnamo Novemba 20, 2021. AP - Petros Giannakouris
Matangazo ya kibiashara

Kupungua huku kwa haki za wanawake kunahatarisha kuwa na madhara makubwa kwa wakazi wote wa Afghanistan, hasa katika upatikanaji wa huduma za afya, elimu na msaada  wa chakula, amebainisha mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF katika kanda hiyo.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, zaidi ya nusu ya wakazi wa Afghanistan wanahitaji msaada wa kibinadamu wakati wa kipindi cha baridi. Mashirika yasiyo ya kiserikali hutoa misaada muhimu, sio tu kupitia misaada wanayotoa, lakini pia kupitia idadi ya kazi wanazotoa. Jumapili hii, wakati mashirika matatu mashuhuri, Save the Children, CARE na shirika linalohudumia Wakimbizi la Norway, yamechukuwa uamuzi wa kusitisha shughuli zao, mashirika mengine kadhaa yamekuwa yakishauriana ili kubaini jibu lao kwa uamuzi wa mamlaka.

"Sio uamuzi ambao tulichukua kwa urahisi, lakini ni mstari mwekundu kwetu. Ili kufanya kazi, tunahitaji usawa kati ya wanaume na wanawake. Ni ssuala ambalo haliwezi kujadiliwa. Hatuwezi kufanya kazi katika mfumo unaobagua nusu ya watu. Hatuwezi kupata maelewano kuhusu hili,” amesema Becky Roby, mkurugenzi wa uwakilishi katika shirika linalohudumia Wakimbizi la Norway.

Wito kwa hatua ya Pamoja kwa mashirika yasiyo ya kiserikali 

Shirika linalohudumia Wakimbizi la Norway limetoa wito kwa mashirika mengine yasiyo ya kiserikali pia kusimamisha kazi ili kuweka uwiano mzuri wa nguvu dhidi ya Taliban. Katika barua waliyotuma kwa mashirika yasiyo ya kiserikali jana, mashirika hayo yaliripoti malalamiko kuhusu wafanyakazi ambao hawakuheshimu sheria za mavazi ya Kiislamu. Ndiyo njia pekee ya kupata matokeo chanya,” anaendelea Becky Roby

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.