Pata taarifa kuu
UKRAINE

Ukraine yaomboleza vifo vya askari 49 baada ya ndege yake kudunguliwa na waasi

Ukraine inafanya maombolezo ya kitaifa leo Jumapili,huku serikali ikiapa kulipiza kisasi dhidi ya waasi wanaounga mkono Urusi, baada ya kudungua ndege ya jeshi la serikali na kuua wafanyakazi 49 katika shambulizi baya kuwahi kutokea dhidi ya vikosi vya serikali mashariki mwa nchi hiyo. 

Mabaki ya ndege ya jeshi la Ukraine iliyodunguliwa na waasi wanaounga mkono Urusi Juni 14 2014.
Mabaki ya ndege ya jeshi la Ukraine iliyodunguliwa na waasi wanaounga mkono Urusi Juni 14 2014. REUTERS/Shamil Zhumatov
Matangazo ya kibiashara

Urusi na Ukraine pia wanakutana kwa mazungumzo muhimu kuhusu gesi leo Jumapili kujaribu kuizuia Urusi kusitisha usambazaji wa gesi yake jambo ambalo litaathiri eneo kubwa la Ulaya.

Duru mpya ya mazungumzo hayo inakuja siku moja baada ya kundi la watu wenye hasira kushambulia na kuvunja madirisha ya ubalozi wa Urusi mjini Kiev na kurusha kifaa chenye uwezo wa kulipua moto katika kuta zake.

Rais mpya wa Ukraine anayeungwa mkono na mataifa ya Magharibi Petro Poroshenko, ameapa kupambana na waasi wanaoiunga mkono Urusi ambao wamewaua askari 49 kwa kuiangusha ndege ya kijeshi katika shambulizi hilo.

Shambulizi hilo limejiri saa kadhaa kabla ya viongozi wa juu wa Urusi na Ukraine kukutana mjini Kiev kwa ajili ya mazungumzo ya saa 11 kuhusu gesi yanayolenga kuepusha usitishwaji wa usambazaji gesi ya Urusi nchini Ukrainejambo ambalo litaathiri pia eneo kubwa la Ulaya.

Tukio hilo la mapema asubuhi limetekelezwa katika mji wa Lugansk ngome kuu ya waasi, siku moja baada ya vikosi vya Ukraine kupata mafanikio makubwa katika kampeni yao kubwa ya Kurejesha pamoja taifa hilo lililogawanyika.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.