Pata taarifa kuu
UGIRIKI-UTURUKI-WAKIMBIZI-USALAMA

Ugiriki yajiandaa kwa zoezi la kwanza la kuwarejesha wahamiaji Uturuki

Kundi la kwanza la wahamiaji ambao watafukuzwa kutoka nchini Ugiriki kwenda Uturuki limewasili katika bandari za Ugiriki za Chios na Lesbos.

Kwenye mpaka wa Makedonia na Ugiriki, wahamiaji wakabiliana na polisi, Ijumaa Agosti 21,2015.
Kwenye mpaka wa Makedonia na Ugiriki, wahamiaji wakabiliana na polisi, Ijumaa Agosti 21,2015. REUTERS/Ognen Teofilovski
Matangazo ya kibiashara

Mamia ya wahamiaji wamesafirishwa katika bandari hizi za visiwa vya Ugiriki kwa basi, hirika la habari la Ufaransa la AFP limearifu. Whamiaji hao watafukuzwaJumatatu leo mchana chini ya mkataba wa mazungumzo kati ya Umoja wa Ulaya na Uturuki.

Makubaliano yaliyofikiwa mwezi uliopita kati ya Umoja wa Ulaya na Uturuki yameanza kutekelezwa rasmi Jumatatu hii Aprili 4, kwa lengo la kuzuia wimbi la wahamiaji kuwasili katika pwani za Ugiriki. Nchini Ugiriki, mamlaka imeanza kundaa maandalizi ya kundi la kwanza litakalorejeshwa nchini Uturuki. Lakini maswali ni mengi kuhusu kukamilia kawa mchakato huu.

Maafisa wa Ugiriki na Ulaya bado hawajaeleza lolote kuhusu jinsi gani zoezi hili litaendeshwa na katika mazingira yapi. Kwa mujibu wa shirika la habari la Ugiriki Ana, wahamiaji 750 wanatazamiwa kusafirishwa katika kisiwa cha Lesbos na bandari Uturuki ya Dikili kati ya Jumatatu na Jumatano.

Tangu Machi 20, tarehe ya kuanza kutumika mkataba huu, baadhi ya watu 6,000 waliingia katika kisiwa cha Lesbos lakini pia Chios, Samos na Leros, visiwa vinne vyenye vituo vya kuorodhesha wakimbizi. Hata hivyo Idara ya Frontex inayofuatilia ulinzi wa mipaka ya nje ya Umoja wa Ulaya, ambayo itasimamia zoezi hili.

Tume ya Ulaya hivi karibuni ilibaini kwamba itawatuma maafisa 4,000 - polisi, wakalimani au maafisa wa ulinzi wa haki ya kupata hifadhi ambao wanaweza kukabiliwa na wimbi la maombi ya hifadhi katika dakika ya mwisho, mkataba unabaini uchunguzi wa kila mtu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.