Pata taarifa kuu

Urusi: Washukiwa wakuu wanne wa shambulio la Moscow wawekwa kizuizini kabla ya kesi

Watuhumiwa wanne waliohusika na shambulio kwenye jumba la tamasha la Crocus City Hall, ambalo lilisababisha vifo vya watu 137 kulingana na ripoti ya hivi punde iliyotangazwa hadharani, waliwekwa kizuizini kwa miezi miwili siku ya Jumapili, Machi 24, na mahakama katika mji mkuu wa Urusi. 

Mshukiwa wa shambulio la jumba la tamasha la Crocus City Hall ameketi nyuma ya ukuta wa kioo wa chumba cha washtakiwa katika Mahakama ya Wilaya ya Basmanny huko Moscow, Urusi, Machi 24, 2024.
Mshukiwa wa shambulio la jumba la tamasha la Crocus City Hall ameketi nyuma ya ukuta wa kioo wa chumba cha washtakiwa katika Mahakama ya Wilaya ya Basmanny huko Moscow, Urusi, Machi 24, 2024. REUTERS - Yulia Morozova
Matangazo ya kibiashara

Wanaume hawa wanne wanatuhumiwa kwa "ugaidi" na wanakabiliwa na kifungo cha maisha, inabainisha taarifa kwa vyombo vya habari kutoka mahakama ya Basmanny huko Moscow. Kizuizi chao cha kabla ya kesi, kilichowekwa hadi Mei 22, kinaweza kurefushwa hadi kesi yao isikilizwe, ambapo tarehe yake bado haijatangazwa.

Mahakama ya Wilaya ya Basmanny mjini Moscow iliwashtaki rasmi Dalerzdzhon Mirzoyev mwenye umri wa miaka 32, Saidakrami Rachabalizoda, 30, Shamsidin Fariduni, 25, na Mukhammadsobir Faizov, 19 kwa kufanya shambulizi la kigaidi la kikundi lililosababisha vifo vya wengine.

Wawili kati ya washukiwa hao walikiri kuhusika na shambulizi hilo baada ya kushitakiwa katika kikao cha awali cha kusikilizwa kesi, kulingana na Taarifa ya mahakama.

Washukiwa hao walionesha dalili za kupigwa wakati walifunguliwa mashitaka ya ugaidi. Mmoja alionekana kabisa kutokuwa na fahamu wakati wa kikao cha kusikilizwa kesi yao.

Idadi kamili ya kura zilizopigwa inahitajika ili kushinda katika duru ya kwanza. Vinginevyo, washindi wawili wa kwanza watashindana katika duru ya pili.

Matokeo yaliyochapishwa kwenye vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii yanamweka mgombea Bassirou Diomaye Faye mbele ya yule wa kambi tawala, Amadou Ba, na kwa mbali sana kuliko wengine.

Angalau wagombea saba kati ya 17 walimpongeza Bw Faye kwa kuzingatia matokeo ya muda yaliyochapishwa na vyombo vya habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.