Pata taarifa kuu

Poland: Bunge kufungua mjadala juu ya upatikanaji wa utoaji mimba

Mjadala unaosubiriwa kwa hamu juu ya kuhalalisha sheria kali za uavyaji mimba nchini Poland, nchi yenye Wakatoliki wengi, unatarajiwa kuanza Alhamisi katika bunge la Poland, huku kukiwa na mgawanyiko katika suala hilo, hata ndani ya muungano unaounga mkono na Umoja wa Ulaya.

Rais wa Poland Andrzej Duda akihutubia Bunge wakati wa kikao cha kwanza cha Bunge jipya mjini Warsaw, Poland, Novemba 13, 2023.
Rais wa Poland Andrzej Duda akihutubia Bunge wakati wa kikao cha kwanza cha Bunge jipya mjini Warsaw, Poland, Novemba 13, 2023. AFP - WOJTEK RADWANSKI
Matangazo ya kibiashara

Poland iliona msukosuko mkubwa katika haki za wanawake wakati wa miaka minane ya utawala wa kihafidhina wa utaifa ambao ulisababisha kupigwa marufuku kabisa kwa uavyaji mimba, na hivyo kuzua mikutano mikubwa ya maandamano.

Kufuatia uchaguzi wa wabunge wa mwezi Oktoba, muungano unaounga mkono Umoja wa Ulaya uliingia madarakani hasa kutokana na ahadi za kurejesha haki za uzazi, ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa utoaji mimba, ambao kwa sasa ni halali tu ikiwa mimba itatokana na kubakwa au kulawitiwa, au ikiwa inatishia maisha moja kwa moja au afya ya mama.

Licha ya ahadi hizi za uchaguzi, maandishi ya rasimu yanayolenga kuziweka huru sheria hizi yamesalia kuzuiwa Bungeni, na hivyo kuibua hasira na kuchanganyikiwa kwa makundi mengi ya wanawake na makundi yanayotetea haki.

Mjadala wa kwanza wa saa sita umepangwa kuanza Alhamisi alasiri.

"Hawa ni wanasiasa ambao walitunyang'anya haki zetu za uzazi, kwa hivyo ni wakati wa kuzirejesha kwetu," Krystyna Kacpura, mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Wanawake na Uzazi wa mpango, ameliambia shirika la habari la AFP.

Muungano wa Kiraia wa Waziri Mkuu Donald Tusk umewasilisha mswada wake wa kuhalalisha uavyaji mimba hadi wiki ya 12 ya ujauzito, na mapendekezo mengine matatu sawia kutoka kwa washirika wake wa muungano pia yanasubiriwa kujadiliwa.

- "Maedeleo madogo" -

Kutokuwa na uhakika kumetawala, hata hivyo, kuhusu matokeo ya mjadala huu wa kwanza, hasa kuhusu uungwaji mkono, wa kutosha au la, ambao miradi hiyo minne inaweza kupata ili kutumaini kupitisha kura ya kwanza iliyopangwa kufanyika siku ya Ijumaa.

"Miswada yenye maudhui sawa ilijadiliwa Bungeni mara nyingi katika kipindi cha miaka thelathini iliyopita (...) hakuna hata mmoja kati yake iliyoweza kupitishwa kupitia kamati," amekumbusha Bw. Kacpura.

Kuidhinishwa rasimu hii siku ya Ijumaa kukuwa "mabadiliko chanya na labda maendeleo madogo," anasema.

Mkuu wa serikali, Donald Tusk, mkuu wa zamani wa Baraza la Ulaya na adui mkubwa wa watangulizi wake katika chama cha Sheria na Haki (PiS), alionyesha "matumaini" kwamba wabunge wa muungano wake wataruhusu rasimu hii mapya kuvuka kikwazo cha kwanza.

"Kuna dalili nyingi (kwamba) itakuwa hivyo," Tusk aliwaambia wanahabari siku ya Jumanne.

Matokeo ya kura, hata hivyo, yako mbali na utabiri.

Wabunge wa chama cha wakulima wa kihafidhina PSL, mwanachama wa muungano huo, wameelezea mashaka yao kuhusu kurahisisha mipango hiyo, huku baadhi yao wakitangaza kuwa hawataunga mkono mipango iliyopendekezwa.

"Nitapiga kura dhidi ya mipango hiyo," Marek Sawicki wa PSL ameiambia redio ya ndani TOK FM, bila kutaja ni wangapi miongoni mwa wenzake watafuata mfano wake.

Ikiwa wengi wanasema hapana, maandiko yana hatari ya kukataliwa na Baraza la Wawakilishi.

- Kutumia kura ya turufu -

Huku usaidizi wa uavyaji mimba ukiwa umepigwa marufuku nchini Poland, wanaharakati na madaktari wanaotoa msaada wanakabiliwa na kifungo jela.

Mwaka jana, mwanaharakati Justyna Wydrzynska alipatikana na hatia ya kutoa tembe za kuavya mimba kwa mwanamke mjamzito na kuhukumiwa kutumikia jamii.

Kulingana na kura ya maoni ya hivi punde iliyofanywa na shirika la  Opinia24, 50% ya Wapolandi wanaunga mkono sheria za utoaji mimba kuwa huria, huku 41% wakisema hawatabadilisha sheria zinazotumika.

Ikiwa bunge litapigia kura mageuzi hayo, bado yatalazimika kusahihishwa na Rais wa Poland Andrzej Duda, mshirika wa PiS na Mkatoliki mwenye msiammo mkali.

Mwezi uliopita, Bw. Duda alipiga kura ya turufu juu ya sheria ya uzazi wa mpango wa dharura, hadi sasa inapatikana tu kwa maagizo, kwa wasichana na wanawake kutoka umri wa miaka kumi na tano, akielezea nia yake ya "kuheshimu haki za kikatiba na viwango vya kulinda afya ya watoto".

Serikali imetangaza tangu wakati huo kwamba itakwepa kura hii ya turufu kwa kuwaidhinisha wafamasia kuagiza wenyewe kidonge cha asubuhi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.