Pata taarifa kuu
UN-MAREKANI-PALESTINA-ISRAELI-Usalama-Siasa

Jitihada za kaimataifa za kusitisha mapigano Gaza zaendelea

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry, ametangaza akiwa Israeli kwamba kuna baadhi ya hatua ambazo zimeshatekelezwa ilikufukia usitishwaji mapigano kati ya Israeli na Hamas katika ukanda wa Gaza.

Wanajeshi wa Israeli wakiingia katika ukanda wa Gaza .
Wanajeshi wa Israeli wakiingia katika ukanda wa Gaza . REUTERS/ Ronen Zvulun
Matangazo ya kibiashara

“ Tumefanya hatua kubwa, lakini inabaki ni vitendo”, Kerry ameambia wanahabari,kabla ya kukutana na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika hoteli moja mjini Jerusalem.

Kerry atakutana jumatano wiki hii na rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas mjini Ramallah na waziri mkuu wa Israeli, Benjamini Netanyahu kwenye wizara ya ulinzi mjini Tel-Aviv, kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema kwamba wanafanya jitihada ili kuhakikisha hali ya utulivu imerejea katika ukanda wa Gaza.
“Tunajaribu kuweka nguvu zetu pamoja ili kuhakikisha pande zote katika mzozo zinakubali kusitisha mapigano”, amesema Ban, huku akibaini kwamba hawana muda wa kupoteza au kusubiri.

Hayo yakijiri, waziri wa Palestina mwenye dhamana ya mambo ya nje, katika kikao cha Baraza la Haki za binadamu mjini Geneva jumatano wiki hii, ameituhumu Israeli kwamba inaendelea kutekeleza uhalifu dhidi ya binadamu katika ukanda wa Gaza.

Katika chumba cha kuhifadhi maiti kwenye hospitali moja mjini Gaza.
Katika chumba cha kuhifadhi maiti kwenye hospitali moja mjini Gaza. REUTERS/Suhaib Salem

“Israeli imekua ikitekeleza uhalifu dhidi ya binadamu. Isareli inaendelea kuharibu na kuteketeza baaji ya miji ya ukanda wa Gaza. Maovu hayo yanayotekelezwa na Israeli ni uhalifu dhidi ya binadamu, na yanakiuka makubaliano ya Geneva”, amesema waziri Riad Malki, ambaye amepongezwa kwa kauli hio na mabalozi wengi waliyoshiriki kikao hicho.

Kwa upande wake mwakilishi wa Israeli kwenye Baraza hilo la Haki za binadamu, Eviatar Manor ameituhumu Hamas kwa kutekeleza uhalifu wa kivita, wakati inaendelea kurusha makombora katika miji inayoikaliwa na watu wa kawaida, huku ikitengeneza barabara za chini ya aridhi kwa kushambulia wakaazi wabaadhi ya vijiji vya Israeli.

Waisraeli wakifurahiwa hatua ya jeshi la Israeli ya kuingia katika ukanda wa Gaza.
Waisraeli wakifurahiwa hatua ya jeshi la Israeli ya kuingia katika ukanda wa Gaza. REUTERS/Nir Elias

“Hamas inahusika na maovu yote yanayotekelezwa katika ukanda wa Gaza, na Abbas anapaswa kuvunja serikali yake ili kuonesha kuwa anaunga mkono mchakato wa amani”, amesema Manor.

Baraza la Umoja wa Mataifa la Hakiza Binadamu linakutana jumatano wiki hii ili kutathmini rasimu ya azimio iliyowasilishwa na Palestina, ambayo imeomba ulinzi wa kimataifa kwa wapalestina na uchunguzi wa haraka wa kimataifakuhusu mashambulizi ya Israeli katika ukanda wa Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.