Pata taarifa kuu
DRC-UNC-Sheria-Siasa

DRC: mbunge wa chama cha upinzani akamatwa

Mbunge kutoka chama cha upinzani cha UNC, Jean-Bertrand Ewanga, amekamatwa mapema jumanne asubuhi, siku moja kabla ya maandamano dhidi ya marekebisho ya katiba, kimethibitisha chama cha UNC. 

Kiongozi wa chama cha UNC, Vital Kamerhe, akikemeya jaribio la kuifanyia marekebisha katiba.
Kiongozi wa chama cha UNC, Vital Kamerhe, akikemeya jaribio la kuifanyia marekebisha katiba. RFI/Bruno Minas
Matangazo ya kibiashara

"Ewanga, ambaye ni katibu mkuu wa chama cha tatu cha upinzani chenye wafuasi wengi, amekamatwa mapema leo asubuhi akiwa nyumbani kwane mjini Knshasa kufuatia mkutano aliyoendesha jumatatu wiki hii", afisa anaehusika na mawasiliano katika chama cha UNC, Lydie Omanga, amesema kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Twitter.

Maelfu ya raia wameandamana jumatatu wiki hii katika mji mkuu wa Congo, Kinshasa dhidi ya marekebisho ya katiba ambayo wanadai kwamba huenda ikampa nafasi rais Joseph Kabila kugombea muhula wa tatu na kusalia madarakani baada ya uchaguzi wa mwaka 2016.

Msichana wa mbunge Ewanga amethibitisha kukamatwa kwa mbunge huyo. “Tunajielekeza kwenye Korti kuu, hapo ndio tutajua yuko wapi”, amesema msichana huyo.

Vyanzo vya familia, vimesema kwamba maafisa wa Idara ya Upelelezi wamewasili nyumbani kwa mbunge Ewanga wakiwa pamoja na askari polisi saa tisa na nusu asubuhi saa za kimataifa.

Katika tangazo liliyotolewa na chama cha UNC,chama hicho kimethibitisha kwamba mbunge Ewanga amepelekwa sehemu isiyojulikana.

“Wameingia nyumbani kwake saa kumi na mbili asubuhi wakiwa na hati ya kumkamata iliyotolewa na muendesha mashtaka, akimtuhumu kukuza chuki. Amepelekwa sehemu ambayo familia yake haijui", kimeeleza chama cha UNC.

Mbunge Ewanga, ni mmoja wa watu waliotoa muhadhara katika maandamano ya jumatatu wiki hii, ambapo amesema kwamba kamwe hawatokubali marekebisho ya katiba.

“Tuna sema tunapinga katiba kufanyiwa marekebisho, ambayo inataka kumpa nafasi rais kusalia madarakani baada ya uchaguzi wa mwaka 2016”, amesema mbunge Ewanga akihutubia umati wa wafuasi wa chama cha UNC waliokua wameshiriki maandamano hayo.

Chama cha UNC kinaongozwa na Vital Kamerhe, aliekua mshirika wa karibu wa rais Joseph Kabila, ambaye kwa sasa anaonekana mpinzani mkuu wa utawala wa rais Kabila.

Rais Kabila alifikia madaraka mwaka 2001, na akachaguliwa katika uchaguzi wa kwanza baada ya kifo cha baba yake mwaka 2006. Mwaka 2011 alichaguliwa kwa muhula wa pili licha ya kuwa ushindi huo ulipingwa na upinzani, na kudai kwamba uligubikwa na wizi wa kura.

Kwa mujibu wa katiba ya nchi, rais Kabila hawezi kugombea muhula wa tatu katika uchaguzi wa mwaka 2016, lakini upinzani unaona kwamba ni mbinu za utawala za kutaka kurekebisha katiba ili impe nafasi ya kugombea.

Rais Kabila anashiriki wakati huu mkutano wa kilele kati ya Marekani na Afrika mjini Washington, Marekani ulimtaka mara kadhaa rais Kabila kuheshimu katiba ya nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.