Pata taarifa kuu
YEMENI-KUBADILISHANA WAFUNGWA

Yemen: Mwanzo wa zoezi la kubadilishana wafungwa kati ya pande hasimu

Majeshi ya serikali ya Yemen na waasi wa Kishia wa Huthi wameanza Jumatano hii zoezi kabambe la kubadilishana mamia ya wafungwa kusini mwa nchi hiyo, kwa mujibu wa afisa aliye karibu na serikali ambaye anatambuliwa na jumuiya ya kimataifa.

Magari ya kivita na mizinga ya majeshi ya nchi za Kiarabu katika Ghuba, Jumanne hii Septemba 8, 2015 katika mkoa wa Marib, kaskazini mwa Yemen.
Magari ya kivita na mizinga ya majeshi ya nchi za Kiarabu katika Ghuba, Jumanne hii Septemba 8, 2015 katika mkoa wa Marib, kaskazini mwa Yemen. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Zoezi hili la kubadilishana wafungwa linafanyika katika siku ya pili ya usitishwaji mapigano kati ya pande husika katika mgogoro, na wakati ambapo mazungumzo ya amani yanafanyika nchini Uswisi tangu Jumanne hii kujaribu kumaliza mgogoro ambao umesababisha tangu mwezi Machi vifo vya watu 6,000.

"Tumeanza zoezi hili la kubadilishana wafungwa kwa makundi madogo", Sheikh Mukhtar al-Rabbach, mjumbe wa Kamati ya wafungwa, amesema.

"Kwa sababu za kiusalama, tumelazimika kugawanya wafungwa katika kundi la watu 20", Mauhktar al-Rabbach ameongeza, na kubaini kwamba wafungwa wamesafirishwa kwa basi.

Zoezi hili linloahusu wafungwa 375 wa waasi na wapiganaji 285 wanaoiunga mkono serikali, limeanzia katika jimbo la Lahej, mashahidi wamesema.

Akihojiwa na shirika la habari la Ufaransa la AFP, mjumbe wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) katika mji wa Sanaa amesema "hana taarifa yoyote kuhusu zoezi hili la kubadilishana wafungwa."

Hii ni moja ya mazoezi machache ya kubadilishana wafungwa yaliotangazwa nchini Yemen tangu muungano wa kiarabu kuingilia kijeshi nchini humo mwishoni mwa mwezi Machi, muungano ambao unaongozwa na Saudi Arabia katika kumsaidia rais Abd Rabbo Mansour Hadi dhidi ya waasi wa Kishia wa Huthi na washirika wao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.