Pata taarifa kuu
UTURUKI-MGOMO

Mahakama ya Uturuki yawafungulia kesi watu wanaoshukiwa kupanga maandamano mwaka jana

Uturuki imewafungulia mashtaka zaidi ya wanaharakati Ishirini kwa kupanga na kuongoza maandamano dhidi ya serikali mwaka uliopita, maandamano yaliogubikwa na vurugu pamoja na ghasia.

Waandamanaji katika mji mkuu Instamboul
Waandamanaji katika mji mkuu Instamboul REUTERS/Osman Orsal
Matangazo ya kibiashara

Mahakama mjini Instanbul imeanza kusikiliza kesi hiyo ambayo waandamanaji hao 26 kutoka vuguvugu la Taksim Solidarity umbrella waliongoza maandamano ya kumshinikiza Waziri Mkuu Recep Tayyip Erdogan kuondoka madarakani baada ya kuongoza nchi hiyo kwa miaka 11.

Waandamanaji hao ambao wamekuwa wakizuiliwa wanawajumusiha Madaktari, Wahandishi na watu wa kawaida ambao wamefunguliwa mashtaka ya kufadhili kundi haramu, kutishia usalama wa taufa hilo na kusambaza ujumbe wa uchochezi dhdi ya serikali kupitia mitandao ya kijamii.

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty Internationale linalaani kufunguliwa mashtaka kwa waandamanaji hao kwa kile inachosema ni serikali kutaka tu kuonesha nguvu na mamlaka yake na ni kesi ambayo imechochewa kisiasa.
Wakati wa maandamano hayo, watu wanane walipoteza maisha na zaidi ya elfu nane wakajeruhiwa.

Ikiwa waandamanaji hao watapatikana na hatia watafungwa jela miaka 29.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.