Pata taarifa kuu
UINGEREZA-EU-USHIRIKIANO

Uingereza: kwa wiki 10 za kupiga kura, kampeni yaanza

Kampeni rasmi kwa kura ya maoni juu ya nafasi ya Uingereza katika Umoja wa Ulaya zinaanza Ijumaa hii Aprili 15, wakati ambapo bado yanasalia majuma kumi tu ili kura hiyo ifanyike.

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron (kushoto)akikutana kwa mazungumzo na Rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk, Februari 18, 2016.
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron (kushoto)akikutana kwa mazungumzo na Rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk, Februari 18, 2016. REUTERS/Yves Herman
Matangazo ya kibiashara

Tafiti zinaonyesha kuwa kura ya ndio na hapana zinasogeleana na itakua vigumu kutabiri matokeo, na kura hii itakua ya kwanza kwa Uingereza narani Ulaya tangu mwaka 1975.

Jumatano wiki hii, Tume ya uchaguzi imeteua kampeni mbili rasmi ambazo zitafanyika hadi Juni 23: Kura inayojulikana kama "Vote Leave", kambi rasmi kwa ajili ya kuondoka kwa Uingereza katika Umoja wa Ulaya, dhidi ya kura nyingine inayojulikana kama "The In Campain" kambi inayounga mkono Uingereza kubaki katika Umoja wa Ulaya.

Uteuzi ramsi ambao unawapa haki ya kutumia kila upande paundi milioni 7 (Euro milioni 8.7), wakati ambapo makundi mengine yatakuwa tu na haki ya kutumia paundi 700,000 kila upande.

Waziri Mkuu David Cameron anaongoza kambi inayounga mkono Uingereza kubaki katika Umoja wa Ulaya, akitetea "sheria maalum" ya Uingereza ndani ya ya Umoja huo alioitilia manani katika mazungumzo ya mwezi Februari pamoja na washirika wake wa Ulaya. Amerejelea kwamba nchi ya Uingereza itakuwa tajiri na yenye nguvu iwapo itabaki ndani ya Umoja wa Ulaya.

Bw Cameron ana imani kwamba kambi yake itapata ushindi hata kama suala mgawanyiko katika chama chake cha Conservative linaendelea kushuhudiwa na licha ya matatizo yake ya hivi karibuni na kupoteza imani kwa wananchi kutokana na kashfa ya ukwepaji kodi.

Itafahamika kwamba vyama vikuu vya siasa na waajiri wengi muhimu nchini humo wametoa msimamo wao wa Uingereza kubaki katika Umoja wa Ulaya.

Shirika la Fedha Duniani (IMF) pia limesema kuwa kujiondoa kwa nchi yoyote katika Umoja wa Ulaya "kunaweza kusababisha madhara makubwa ya kikanda na kimataifa na kuvuruga mahusiano ya biashara yaliyokua yakiendelea vizuri."

Siku ya Alhamisi, kiongozi wa chama cha Labor, Jeremy Corbyn, alitoa hotuba yake kuu ya kwanzainayounga mkono Uingereza kubaki katika Umoja wa Ulaya. Kiongozi huyu anaweza kuwa na jukumu muhimu kwa kuwashawishi wapiga kura, hasa vijana, kupiga kura katika neema ya Uingereza kubaki katika Umoja wa Ulaya, waangalizi wa mambo wanasema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.