Pata taarifa kuu
DRC-UN-Usalama

DRC: UN yatiwa hofu na mdororo wa kiusalama katika baadhi ya maeneo

Umoja wa mataifa nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya kongo Drc, unasema kuwa licha ya majeshi ya MONUSCO na yale ya serikali kufanikiwa kwa sehemu kubwa kukomesha uasi mashariki mwa nchi hiyo, bado changamoto za kiusalama zimeendelea kusalia.

Mkuu wa tume ya MONUSCO akiwa pia mwakilishi maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa , Martin Kobler, akiwasabahi wanajeshi wanawake wa Congo.
Mkuu wa tume ya MONUSCO akiwa pia mwakilishi maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa , Martin Kobler, akiwasabahi wanajeshi wanawake wa Congo. Monusco/Myriam Asmani
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa tume ya MONUSCO nchini DRC, Martin Kobler akiwahutubia wajumbe wa baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa alhamisi jioni wiki hii, amesema kuwa hivi sasa hali ya usalama mashariki mwa DRC ni yakurudhisha kutokana na juhudi ambazo zimekuwa zikifanywa na vikosi vya Serikali pamoja na majeshi ya MONUSCO.

Makundi kadhaa ya waasi yamekuwa yakifanya uasi mashariki mwa nchi hiyo wakiwemo waliokuwa waasi wa M23, waasi wa kihutu wa FDLR pamoja na waasi wa Uganda wa ADF-NALU.

Martin Kobler amesema kuwa katika kipindi cha miezi 12 iliyopita, hali ya mambo imebadilika nchini humo.

Hayo yakijiri waanadiplomasia wa Umoja wa Ulaya walioko mjini Kinshasa- Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameelezea wasiwasi wao baada ya kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani Jean Bertrand Ewanga, Mbunge na Katibu mkuu wa chama cha upinzani cha UNC cha bwana Vital Kamerhe siku ya Jumanne tarehe 5 mwezi Agosti mwaka huu.

Mabalozi hao, Luc Hallade wa Ufaransa, Michel Latshenko wa Ubelgiji, na Naibu Balozi wa Uingereza, John Lamb, kwa pamoja wamebaini wasiwasi wao kwa spika wa Bunge nchini DRC Aubin Minaku na kutoa wito kwa serikali ya Congo kuchukua hatua mahususi ili kutowa uhuru na haki ya kujieleza, kama alivyobaini Bruno Hanses anayeshughulikia Mambo ya Ndani ya Ujumbe wa Umoja wa Ulaya mjini Kinshasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.