Pata taarifa kuu
Tanzania-Katiba

Bunge maalum la katiba nchini Tanzania laahirisha vikao vyake hadi alhamisi ijayo

Bunge maalumu la Katiba nchini Tanzania limeendelea tena leo asubuhi kabla ya kuahirishwa hadi siku ya alhamisi ya juma lijalo, wakati huu bado kukiendelea kushuhudiwa mivutano ndani ya kamati zilizoundwa na mwenyekiti.

Wabunge wa Bunge la Katiba nchini Tanzania wakisikiliza hotuba ya rais Kikwete
Wabunge wa Bunge la Katiba nchini Tanzania wakisikiliza hotuba ya rais Kikwete issamichuzi.com
Matangazo ya kibiashara

Hali ya mvutano i,eshuhudiwa wakati wa kikao cha leo asubuhi cha bunge maalumu katiba nchini Tanzania, ambapo punde mara baada ya kuwasilishwa kwa mapendekezo ya kufanyiwa marekebisho ya kanuni za bunge na kuungwa mkono baadhi ya wajumbe walisimama wakipinga hatua hiyo.

Dalili za kujitokeza mvutano ndani bunge zilianza mapema baada ya kuwasilishwa kwa hoja ya kufanya mabadiliko ya kanuni na makamu mwenyekiti kuruhusu mjadala kuhusu pendekezo lililowasilishwa na kamati ya kanuni na haki za bunge, hali ambayo wajumbe toka vyama vya upinzani walipinga.

Lakini katika kile kilichoonekana ni kauli ya ujasiri na hata kupongezwa na wajumbe wengi wa bunge maalumu, ni kauli aliyoitoa mbunge wa upinzani Felix Mkosamali ambaye aliwataka wenzake kutopinga masuala madogo na badala yake kuwa na misimamo kwenye masuala ya msingi.

Kufuatia mjadala kuonekana unachukua muda ndipo baadhi ya wabunge wakataka makamu mwenyekiti atumie madaraka yake kuwahoji wabunge iwapo wanaunga mkono au la, hatua ambayo wakati makamu mwenyekiti Samia Suluhu akitaka kuwahoji wabunge mjumbe mmoja alisimama na kupinga maamuzi hayo.

Hata hivyo licha ya kuzuka kwa zogo, baadae wajumbe waliunga mkono Hoja na kisha mwenyekiti kuahirisha kikao cha leo hadi alhamisi ya Juma lijalo ambapo kamati zitapata nafasi ya kuwasilisha ripoti zao kuhusu mijadala ya sura mbili za rasimu walizopewa kuzijadili.

Katika hatua nyingine mwenyekiti wa bunge maalumu, alitangaza kuongeza wajumbe wengine wa tano kwenye kamati ya ungozi, kamati ambayo awali ililalamikiwa kwakuwa na wajumbe toka upande mmoja.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.