Pata taarifa kuu
YEMENI-MAPIGANO-USALAMA-SIASA

Yemen: vita vyarindima

Wahusika wakuu wa mgogoro nchini Yemen watakutana tena kwa mazungumzo mnamo Januari 14 baada ya raundi ya kwanza ya mazungumzo yaliosimamiwa na Umoja wa Mataifa, na kumalizika Jumapili hii nchini Uswisi huku kukiwa na kuendelea kushuhudiwa ukiukwaji wa mkataba wa usitishwaji wa mapigano.

Wanamgambo wanaounga mkono jeshi la serikali inayotambuliwa kimataifa, katika mji wa Sirwah, Yemen, Desemba 18, 2015.
Wanamgambo wanaounga mkono jeshi la serikali inayotambuliwa kimataifa, katika mji wa Sirwah, Yemen, Desemba 18, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

"Tumeamua kukutana katika raundi ya pili ya mazungumzo Januari 14", amesema mjumbe wa Umoja wa Mataifa, Ismail Ould Cheikh Ahmed, wakati wa mkutano naa waandishi wa habari mjini Bern, bila hata hivyo kufafanua eneo kutakapofanyika mazungumzo hayo.

"Tumefanya maendeleo makubwa lakini hayajatosha", amesema mjumbe wa Umoja wa Mataifa, akiainisha matokeo ya mazungumzo ya amani yaliofanyika katika kikao cha faragha tangu Jumanne Desemba 15 kati ya wawakilishi wa serikali inayotambuliwa kimataifa na waasi wa Kishia wa Huthi katika kujaribu kukomesha vita hivyo ambavyo vimedumu sasa karibu miezi tisa.

Ismail Ould Cheikh Ahmed ametangaza kwamba kumefanyika "makubaliano" juu ya kuundwa kwa "tume ya mawasiliano na kutuliza vita, linalojumuisha washauri wa kijeshi wa pande zote mbili na kusimamiwa na Umoja wa Mataifa" pamoja na utekelezaji wa "hatua za matumaini, ikiwa ni pamoja na kuachiliwa huru kwa mahabusu na wafungwa. "

Ameongeza kuwa ameendelea kufanya mashauriano na pande tofauti kwa kongeza muda wa mkataba wa usitishwaji wa mapigano, lakini mkataba huo umekua ukikiukwa mara kwa maratangu kuanza kutekelezwa Jumanne Desemba 15 na ambao unatazamiwa kumalizika Jumatatu hii jioni.

"Lengo ni kufikia mkataba wa jumla wa kusitisha mapigano na ambao utaheshimishwa na pande zote", alisema mjumbe wa Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.