Jukwaa la Michezo
Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.
Soma yanayofuataSikiliza kipindi kilichopita
Vipindi vyote
-
AFCON 2024: Michuano ya hatua ya 16 bora kuanza
Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na michuano ya hatua ya 16 kuwania taji la soka kwa mataifa ya bara Afrika. Mashindano ya mchezo wa mikono bara Afrika yanayoendelea kule Misri na Aryna Sabalenka kushinda mashindano ya Australian Open kwa upande wa wanawake.27/01/202423:49 -
Mataifa ya Afrika yaendelea kupambana kutafuta taji la AFCON
Tunaendelea kukuletea uchambuzi wa michuano ya soka kuwania ubingwa kwa mataifa ya Afrika, inayoendelea nchini Cote Dvoire. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Tanzania, pia zinapambana kuwania taji hilo. Ungana na wachambuzi wetu Jason Sagini, George Ajowi na Jason Sagini akiwa mjini San Pedro.20/01/202423:56 -
Michuano ya AFCON yaanza nchini Cote Dvoire, nani ataibuka mshindi ?
Michuano ya soka kuwania taji la mataifa ya Afrika maarufu kama AFCON, inaanza leo nchini Cote Dvoire. Hii ni mara ya kwanza kwa mashindano haya makubwa kurejea kwenye nchi hiyo ya Afrika Magharibi kwa mara ya kwanza baada ya miaka 40. Kuna timu 24 zinazotafuta ubingwa wa taji hili, ikiwemo Taifa Stars ya Tanzania na Leopard ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutoka Afrika Mashariki na Kati. Wachambuzi wetu Paul Nzioki, George Ajowi na Jason Sagini, akiwa Abidjan, wnachambua.13/01/202423:50 -
CAF yaongeza kiwango cha fedha kwa mshindi wa AFCON 2024
Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF kuongeza kiwango cha fedha kwa mshindi wa michuano ya AFCON, itakayoanza Januari 13 nchini Cote Dvoire, Bondia wa DRC Martin Bakole aomba mchango wa fedha kushiriki mechi za mkanda wa WBA, matokeo ya Mapinduzi Cup na kombe la Amani visiwani Zanzibar na Brazil yamfuta kazi kocha Fernando Diniz.06/01/202423:56 -
Timu za Afrika zaanza kutangaza vikosi kuelekea AFCON 2024
Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa vikosi vya mwisho vilivyotangazwa na mataifa kadhaa kuelekea AFCON ya mwaka 2023 itakayoanza Januari 13, 2024, raia wa Rwanda Clare Akamanzi ateuliwa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa NBA Africa, Guy Bukasa atangazwa kocha mpya wa AS Kigali, rais wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach atangaza mikakati ya kujumuisha michezo ya kielektroniki e-sports kwenye Olimpiki na kocha Carlo Ancelotti atia saini mkataba mpya klabuni Real Madrid.30/12/202323:54 -
Kenya yaibuka bingwa wa mashindano ya Tong Il Moo Do
Tuliyokuandalia ni pamoja na Kenya kuhifadhi taji lake la Tong Il Moo Do kwa mara ya 11, mkenya Angella Okutoyi ashinda dhahabu mbili kwenye tenisi ya kimataifa ya W25, uchambuzi wa matokeo ya mechi za Klabu bingwa Afrika wiki hii, Man City kutwaa ubingwa wa Kombe la Klabu bingwa Duniani kwa mara ya kwanza na Mahakama ya Ulaya kupinga uamuzi wa FIFA na UEFA kuzuia kuanzishwa kwa Ligi mpya ya Ulaya kuwa kinyume na sheria.23/12/202323:50 -
Mashindano ya Kimataifa ya Tong-Il-Moo-Do yafanyika nchini Kenya
Kenya yaandaa makala ya 11 ya michuano ya kimataifa ya mchezo wa Tong-Il-Moo-Do jijini Mombasa. Uganda ndio washindi wa CECAFA katika mechi za kufuzu kwa michuano ya CAF ya Shule za Afrika. Al Ahly waishinda Al-Ittihad kutinga Nusu Fainali ya Kombe la Dunia la Vilabu Kisha Paris Saint - Germain yatinga hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa.16/12/202321:01 -
Messi ashinda tuzo ya Ballon d'Or tena
Miongoni mwa yale tunayojadili ni pamoja na tuzo za wachezaji bora barani Afrika mwaka huu katika mchezo wa soka, timu ya taifa ya Uganda Cranes kupata kocha mpya, mechi za soka kufuzu michezo ya Olimpiki Paris 2024 miongoni mwa wanawake, Lionel Messi kushinda tuzo ya nane la Ballon d'Or, miongoni mwa mengine.04/11/202323:50 -
Uchaguzi wa viongozi wa mchezo wa Tennis barani Afrika
Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na Afrika kupata viongozi wapya wa Shirikisho la mchezo wa Tenisi, uchambuzi wa fainali ya kombe la dunia la raga, pigano la ndondi kati ya Tyson Fury na Francis Ngannou, mechi za kufuzu olimpiki ya mwaka kesho kwa kina dada, Ligi Kuu ya soka Afrika, debi la Manchester na El Clasico na mchezaji wa Newcastle Sandro Tonali kupigwa marufuku ya miezi kumi kwa kujihusisha na masuala ya michezo ya bahati nasibu.28/10/202323:39 -
Raga: Afrika Kusini na New Zealand kuchuana fainali ya kombe la dunia
Tumekuandalia uchambuzi kuhusu fainali inayotarajiwa kati ya Afrika Kusini na New Zealand, kuwania taji la kombe la dunia katika mchezo wa raga lakini pia kuendelea kwa michuano mipya ya soka ya ligi ya Afrika.22/10/202323:52 -
CAF yatangaza droo ya hatua ya makundi, michuano ya klabu bingwa na Shirikisho
Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na uchambuzi wa droo ya hatua ya makundi ya michuano ya klabu bingwa Afrika, Gor Mahia yaibuka na ushindi kwenye debi la mashemeji, uchambuzi wa matokeo ya mechi za klabu bingwa ulaya, Kombe la Dunia la mwaka 2030 kuandaliwa kati ya mataifa sita na Pogba kupatikana ametumia dawa za kusisimua misuli katika kipimo cha pili.07/10/202323:53 -
Afrika Mashariki kuwa wenyeji wa AFCON 2024
Miongoni mwa tuliyokuandalia ni pamoja na Afrika Mashariki kuteuliwa kuandaa Kombe la Mataifa ya Afrika ya mwaka 2027, hatua ya mwisho ya kufuzu Kombe la Mataifa ya wanawake mwaka 2024, raundi ya mwisho kufuzu hatua ya makundi michuano ya klabu bingwa barani Afrika na Kombe la dunia la raga, linaloendelea nchini Ufaransa.30/09/202323:32 -
Mkenya Eliud Kipchoge ashinda tena taji la Berlin Marathon
Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na mwanariadha kutoka Kenya, Eliud Kipchoge kushinda mashindano ya riadha ya Berlin Marathon kwa mara ya tano, Kocha wa timu ya taifa ya wanawake ya Rwanda, asimamishwa kazi ni miongoni mwa mengine mengi yanayotokea viwanjani.24/09/202323:53 -
Klabu za Afrika zachuana kunyakuwa taji la klabu bingwa
Miongoni mwa yale tuliyokuandalia ni pamoja na mahojiano kuhusu kongamano la kibiashara la soka barani Afrika, lililofanyika wiki hii jijini Nairobi. Misri waibuka washindi wa kombe la mataifa ya Afrika voliboli ya wanaume, APR ya Rwanda yashinda ubingwa wa ligi kuu ya basketboli, uchambuzi wa mechi za kufuzu klabu bingwa barani Afrika na kombe la dunia la raga.16/09/202323:55 -
Kombe la dunia la mchezo wa raga, laanza nchini Ufaransa
Tuliyokuandalia ni pamoja na kuanza kwa Kombe la Dunia katika mchezo wa raga nchini Ufaransa, Tanzania kufuzu Kombe la mataifa ya Afrika mchezo wa soka mwaka 2023 na Rwanda yaondolewa kwenye mashindano ya voliboli barani Afrika.09/09/202323:49
Jukwaa la Michezo
Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.