Pata taarifa kuu

Julian Assange apewa haki ya kukata rufaa dhidi ya hatuwa ya kurejeshwa Marekani

Mahakama Kuu mjini London imetoa uamuzi wake siku ya Jumanne Machi 26 kuhusu ombi la Julian Assange la kuweza kukata rufaa dhidi ya kurejeshwa kwake Marekani. Mwanzilishi wa WikiLeaks anaweza kupinga kurejeshwa kwake nchini Marekani, inasema Mahakama Kuu ya Uingereza.

Mwanzilishi wa WikiLeaks Julian Assange mjini London mnamo Jumatano, Mei 1, 2019.
Mwanzilishi wa WikiLeaks Julian Assange mjini London mnamo Jumatano, Mei 1, 2019. AP - Matt Dunham
Matangazo ya kibiashara

Mahakama Kuu mjini London imetangaza siku ya Jumanne kwamba Julian Assange, mwanzilishi wa WikiLeaks, ataweza kukata rufaa dhidi ya kurejeshwa kwake Marekani. Uamuzi wa kurejeshwa nchini Marekani uliidhinishwa na serikali ya Uingereza mnamo mwaka 2022.

Majaji wametoa muda wa wiki tatu kwa mamlaka ya Marekani, ambayo inataka kumhukumu raia huyo wa Australia mwenye umri wa miaka 52 kwa uvujaji mkubwa wa nyaraka za siri, kutoa dhamana. Nchi italazimika kutoa "dhamana ya kuridhisha" kwamba Julian Assange ataweza kuomba marekebisho ya kwanza ya Katiba ambayo inalinda uhuru wa kujieleza na kwamba asiwezi kuhukumiwa adhabu ya kifo.

"Ikiwa uhakikisho huu hautatolewa" ndani ya muda huu wa mwisho, Julian Assange ataweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa kumrejesha nchini Marekani, uliotolewa mwezi Juni 2022 na serikali ya Uingereza, majaji Victoria Sharp na Jeremy Johnson wameamua.

Ikiwa hili litapasishwa, kesi mpya itasikizwa mnamo Mei 20 kabla ya majaji kuamua ikiwa watapata dhamana hizi kuwa za kuridhisha, kuamua ikiwa Julian Assange anaweza kunufaika na uamuzi wa mwisho nchini Uingereza, katika kesi ambayo imekuwa ishara ya vitisho dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari.

Wafuasi wa Julian Assange kwa vyovyote vile walikuwa wameonya kwamba, iwapo watashindwa, watalipeleka suala hilo kwenye Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu kwa matumaini ya kuahirishwa kwa kesi hiyo.

Julian Assange anakabiliwa na kifungo cha miaka 175 jela kwa kuchapisha, kuanzia mwaka 2010, zaidi ya nyaraka 700,000 za siri kuhusu shughuli za kijeshi na kidiplomasia za Marekani, hasa nchini Iraq na Afghanistan. Miongoni mwa nyaraka hizi ni video inayoonyesha raia, wakiwemo waandishi wawili wa habari wa shirika la habari la Reuters, waliuawa kwa shambulio la anga la helikopta ya kivita ya Marekani nchini Iraq mwezi Julai 2007.

Julian Assange alikamatwa na polisi wa Uingereza mwaka 2019 baada ya miaka saba kukaa katika ubalozi wa Ecuador mjini London ili kuepuka kurejeshwa nchini Sweden katika uchunguzi wa ubakaji, uliotupiliwa mbali mwaka huo huo.

Sauti nyingi zimemtaka Rais wa Marekani Joe Biden kufuta mashtaka 18 dhidi ya Bw. Assange wakati wa muhula wa kwanza wa Donald Trump, chini ya sheria ya kijasusi ya mwaka 1917. Katika wiki za hivi karibuni, walio karibu na Julian Assange, aliyezuiliwa kwa miaka mitano katika gereza lenye ulinzi mkali la Belmarsh mjini London, walionya kuhusu kuzorota kwa hali yake ya afya. Utetezi wake pia unaonyesha hatari ya kujiua katika tukio la kurejeshwa nchini Marekani. Katika kesi za mwezi waFebruari, hakuwepo, kutokana na hali yake afya kuzorota.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.