Pata taarifa kuu
UFARANSA-MAANDAMANO-KILIMO

Wakulima wenye hasira waelekea Paris kwa maandamano

Wakulima wa Ufaransa wana hasira na wamekua wakielezea ghadhabu yao. Wakulima hao wanatazamiwa Alhamisi wiki hii kuandamana kwa wingi wakiwa na matrekta yao hadi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Paris.

Trekta karibu na mji wa Caen ikielekea katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris kwa ajili ya kushiriki katika maandamano ya wakulima leo Alhamisi Septemba 3, 2015.
Trekta karibu na mji wa Caen ikielekea katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris kwa ajili ya kushiriki katika maandamano ya wakulima leo Alhamisi Septemba 3, 2015. AFP PHOTO / CHARLY TRIBALLEAU
Matangazo ya kibiashara

Wakulima kutoka wilaya 12 watashiriki katika maandamano hayo katika eneo la taifa. Ujumbe wa wakulima hao utapokelewa leo mchan katika mji wa Matignon, na mwingine utakwenda Bungeni ili kufikisha malalamiko yake kwa wabunge. Maandamano haya yenye ushawishi mkubwa yametajwa kuwa ya kihistoria na wafugaji wengi.

Wakulima wanaelekea kwanza katika mji wa Paris ili waweze kutambuliwa. Wanahisi kwamba hawaeleweki na wamekua wakipuuzwa, na raia watambuwe shida na maisha duni yanayokumba wakulima.

" Kwenda Paris ni pigo kubwa. Kuna matrekta 1500, kutakuwa na zaidi ya watu elfu 4 hadi elfu 5 mchana huu katika eneo la taifa. hali hii inaonyesha dhiki, shida ya wakulima. Leo tunahitaji ufumbuzi wa kweli ambao ni endelevu kwa ajili ya kutupa upya mitazamo na kutupongeza kwa kuamka asubuhi na kufanya bidhaa bora za kilimo ", amesema Luc Smessaert, makamu wa rais wa wa Shirikisho la Wakulima nchini Ufaransa (FNSEA).

Viwango

Mzozo huo pia una sababu zaidi ya kiuchumi na kijamii. Bila shaka, wakulima hawa hawategemei kitu cha ajaabu, lakini wanataka ufumbuzi katika madai yao. Miongoni mwa madai yao, wanaiomba serikali punguzo la gharama ya kazi wanaoifanya na gharama za wafanyakazi. Hizo ni moja ya pointi muhimu.

Ufaransa inaendesha shughuli hii ya kiliomo kwa viwango wakati majirani zake, Ujerumani na Hispania huzalisha kwa nafu na kuuza zaidi nje.

" Serikali inapaswa kujitoa kwa kimuundo, na kutupunguzia mzigo wa gharama na kutupunguzia pia viwango vya ilivyoweka. Na kusema kwamba nafasi kwa Ufaransa ni kuwa na mifugo yenye maziwa, ng'ombe na nguruwe ", amesisitiza Thierry Roquefeuil, rais wa Shirikisho la kitaifa la Uzalishaji wa Maziwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.