Pata taarifa kuu
UINGEREZA-DRC-USHIRIKIANO

Uingereza yatazamia kupitia upya ushirikiano wake na DRC

Serikali ya Uingereza imesema kuwa iko tayari kupitia upya ushirikiano wake na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kabla ya mwishoni mwa mwaka 2016, ikiwa uchaguzi wa rais katika nchi hiyo utafanyika kwa mujibu wa Katiba ya nchi hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila. AFP PHOTO/ALAIN WANDIMOYI
Matangazo ya kibiashara

Kauli hiyo imetolewa Jumanne wiki hii na Mjumbe Maalum wa Uingereza kwa Ukanda wa Maziwa Makuu Danae Dholakia katika mkutano na wandishi wa habari na kubainisha kuwa Uingereza inafikiria kutumia njia zote ikiwa itaona viashiria vya kuahirishwa kwa uchaguzi au marekebisho ya katiba.

Mjumbe huyo amesisitiza kuwa ikiwa Uingereza itabaini hatua zozote za kukiuka taratibu na sheria zilizowekwa, jambo ambalo ni hatari kwa nchi ya DRC, basi watalazimika kutafakari kuhusu misaada yao kwa DRC ambapo serikali ya London ni ya pili kwa ukubwa wa misadaa baina kwa bajeti ya serikali ya Congo kwa mchango wa Euro milioni 1.4 kwa siku.

DRC inakabiliwa na mgogoro wa kisiasa tangu uchaguzi wa Rais Joseph Kabila mwaka 2011 katika uchaguzi uliogubikwa na dosari nyingi, huku Upinzani ukiendelea kushutumu Rais Kabila aliye madarakani tangu mwaka 2001,kutaka kwa njia zote kuwania muhula wa tatu kinyume na Katiba iliopo.

Mwanzoni mwa mwezi Novemba mwaka huu, Rais Kabila alitangaza nia yake ya kuitisha mazungumzo ya kitaifa ili uchaguzi ufanyike kwa amani katika nchi hiyo, ambapo tayari vyama kadhaa vya upinzani vimetangaza kususia mazungumzo hayo vikibainisha kuwa ni mbinu ya rais huyo kutaka kuahirisha uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.